BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWIGIZAJI WA FILAMU KIWANGO CHA DUNIA ALIYEFUNGWA KWA KUWAUA SWALA WATATU AACHILIWA HURU


Mmoja wa nyota wakuu wa kuigiza filamu nchini India, Salman Khan, ameachiliwa na mahakama moja kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mnyama wa mwituni aliye katika hatari ya kuangamia kabisa duniani.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kuwaua swara watatu katika jimbo la Kaskazini la Rajasthan mwaka wa 1998. Mwaka uliopita aliachiliwa na mahakama kwa kosa jingine la kumkanyaga na kumuua mtu asiye na makaazi.

Salman Khan, ni nyota wa filamu kutoka kundi la waigizaji la India, maarufu Bollywood, ambaye ana sifa ya kujikuta mashakani mara kwa mara.
Mwaka 1998 alilaumiwa na kabila moja la Rajasthan kwa kupiga risasi na kuwaua swara watatu wakati alipokuwa katika shughuli za uwindaji.

Swara hao wanalindwa kisheria na pia wanasujudiwa na kabila lililoshtaki.

Alikuwa amepatikana na kosa na mahakama ya chini na kuhukumiwa kifungo lakini sasa ameachiliwa baada ya kukata rufaa.

Mwaka uliopita, nyota huyo anayejipata mashakani mara kwa mara aliachiliwa na mahakama kwa kosa la kumkanyaga kwa gari mtu asiye na makaazi alipokuwa akiendesha gari lake.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: