BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKE WA BILIONEA ERASTO MSUYA WA ARUSHA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MASHTAKA YA MAUAJI YA DADA WA MUME WAKE

Mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, marehemu Bilionea Erasto Msuya, Minam Msuya, akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

MIRIAM Stephen Mrita maarufu kama Miriam Elisaria Msuya (41), ambaye ni mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya dada wa mfanyabiashara huyo, Aneth Elisaria Msuya.

Miriam ambaye ni mkazi wa Sakina kwa Iddi jijini Arusha, alisomewa jana mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Magreth Bankika.

Wakili wa Serikali Diana Lukondo alidai kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Kibada, Wilaya ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua kwa makusudi Aneth Msuya.

Kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapaokamilika na kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Lukondo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu aliamuru mshtakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 6, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa. Miriam alikamatwa Agosti 4, mwaka huu jijini Arusha kabla ya kupandishwa mahakamani jana kwa tuhuma za mauaji ya dada wa bilionea Msuya.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: