By Juma Mtanda, Mwananchi
Morogoro. Kasi ya utumbuaji majipu kwa watumishi wa Serikali imeendelea baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Kessy Mkambala kuwasimamisha kazi watumishi 10 kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa kanuni za uwajibikaji kazi.
Akizungumza na Mwananchi wilayani Kilosa, Mkambala alisema watumishi hao amewasimamisha kazi kwa kutokufuata kanuni na sheria mbalimbali za kiutendaji na hivyo kuisababishia hasara serikali.
Mkambala amesema kati ya watumishi hao waliosimamishwa kazi yupo mkuu wa idara ya manunuzi ya halmashauri hiyo, Geofrey Njovu kwa madai ya kufanya manunuzi yasiyofuata taratibu na kuisababishia halmashauri hasara ya mamilioni ya fedha.
Hata hivyo, Njovu alisema ni vyema Takukuru ikahusishwa kuchunguza tuhuma zinazomkabili kwani hazina ukweli wowote.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ MKURUGENZI MTENDAJI KILOSA AWATUMBUA MAJIPU WATUMISHI 10 KWA KUWASIMAMISHA KAZI MOROGORO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment