BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NDEGE KUBWA ZAIDI DUNIANI YAPATAA AJALI SIKU CHACHE BAADA YA MAJARIBIO YA KURUKA ANGANI

 
Ndege ndefu zaidi duniani - Airlander 10 - imeharibika baada ya kuanguka ikitua kwenye safari yake ya pili ya kufanyiwa majaribio.

Ndege hiyo ya urefu wa 302ft (92m) - ambayo kwa kiasi fulani ni ndege na pia kwa kiasi fulani puto - iliharibika ikiwa katika uwanja wa Cardington, Bedfordshire nchini Uingereza.

Ndege hiyo ya thamani ya £25m imeharibika eneo wanamoketi marubani baada ya kuangika kwa 'pua' mwendo wa saa tano saa za Uingereza.

Msemaji wa HAV, kampuni iliyounda ndege hiyo, amesema marubani na wahudumu wengine wote wako salama.

Kampuni hiyo imekanusha madai kwamba waya uliokuwa umening'inia kutoka kwenye ndege hiyo ulikwama kwenye kigingi cha nyaya za simu na kusababisha ajali hiyo.

Ndege hiyo ilifanya safari yake ya kwanza 17 Agosti.

Airlander 10 kwa takwimu
44,100 lbs (20,000kg): Uzani wa ndege hiyo
20,000ft (6,100m): Umbali ambao inaweza kupaa juu angani
80 knots (148km/h): Kasi yake ya juu zaidi
Siku 5: Muda ambao inaweza kukaa angani
22,050 lbs (10,000kg): Uzani ambao inaweza kubeba.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: