BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS DK MAGUFULI AMPANDISHA CHEO MKUU WA WILAYA KUWA MKUU WA MKOA ARUSHA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua  Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.Chanzo/MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: