BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CUF YANG'ANG'ANIA MGOMBEA WAKE ALIIBUKA MSHINDI UCHAGUZI MKUU 2015

Chama cha Wananchi (CUF), kimeendelea kudai kuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad alishinda na kunyang’anywa ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Akizungumza mjini hapa jana, Maalim Seif ambaye pia ni katibu mkuu wa chama hicho, amesema hakuna namna yoyote watawala wataweza kuzuia haki ya uamuzi wa Wazanzibari walioutoa Oktoba 25, 2015, lakini kinachoendelea ni njama za kuichelewesha.

Maalim amesema hayo wakati akitoa salamu kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliofika kwenye ibada ya Ijumaa katika Msikiti wa Biziredi. CUF wanalalamikia ushindi huo zikiwa zimepita siku 215 tangu uchaguzi wa marudio ulipofanyika Zanzibar.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: