BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAKOCHA WA TIMU YA NETIBOLI YA POLISI MORO WAUMIZA VICHWA ASUBUHI NA JIONI UWANJA WA JAMHURI

Mchezaji wa timu ya netiboli ya Polisi Morogoro, Lidya Joseph akiwatoroka adui zake, Aziza Itonya kulia na, Zainabu Mfyule kushoto wakati wa mazoezi ya maandalizi ya kujiandaa na ligi kuu ya muungano itayofanyika jiji Dar es Salaa mwezi ujao, yaliyofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro. Juma Mtanda.

Juma Mtanda, Morogoro.
Timu ya netiboli ya Polisi Morogoro ipo katika maandalizi makali ya kujiwinda na ligi Kuu ya Muungano ya Netiboli 2016/2017 huku makocha wa timu hiyo wakiumiza vichwa kwa kuyafanyia kazi mambo matatu asubuhi na jioni kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro. 


Akizungumza na MTANDA BLOG mjini hapa, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Oliver Nambunga alisema kuwa yeye na kocha mkuu, Edson Chitanda wapo makini katika kufundisha mambo tatu ili kufanya vyema kwenye michezo ya ligi hiyo na ndoto yao kubwa ni kutwaa ubingwa huo mwaka huu. 


Nambunga alisema kuwa timu ya netiboli ya Polisi Morogoro ina kikosi kizuri chenye wachezaji wenye viwango vya juu vya mchezo huo na wanataka kufanya vizuri lakini michezo ya ligi hiyo itakuwa kama sehemu ya kufanya marekebisha ya makosa yaliyojitokeza katika mashindano ya netiboli ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 hasa mchezo wa mwisho dhidi ya Uhamiaji. 


“Tunawanoa vijana wetu katika mambo matatu ya ufundi na mbinu za mchezo na mojawapo ni pamoja na kukaba maadui, mbinu ya kushambulia na mbinu ya kufunga kwani mashindano ya netiboli ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 tulifanya vizuri kwa kushika nafasi ya pili na sasa tunautaka ubingwa wa ligi kuu ya netiboli ya muungano.”alisema Nambunga. 


Nambunga alisema kuwa watafanya usajili wa maana na kuhakikisha kikosi kinakuwa na ushindani wa hali ya juu katika michezo yote dhidi ya wapinzani wao ambapo ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi katika jiji la Dar es Salaam kati ya Novemba mosi na tano ikishirikisha timu jumla ya timu 10, sita kutoka Tanzania bara na timu nne kutoka Zanzibar. 


Kwa Tanzania bara itawakilishwa na timu sita zilizoshika nafasi ya kwanza hadi sita katika mashindano ya netiboli ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 yaliyofanyikia Morogoro ambapo timu ya Uhamiaji ilitwaa ubingwa huo.

Timu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo ya Muungano ni pamoja na Polisi Morogoro, Jeshi Stars, Madini Arusha, Tumbaku Morgoro na Polisi Arusha.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: