BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBWA AZIKWA AKIWA HAI NA MSUMARI KICHWANI

Mbwa azikwa akiwa hai huku akiwa amedungwa msumari kichwani
Mbwa mmoja amepatikana amezikwa akiwa hai huku msumari ukiwa umedungwa kichwani mwake katika eneo la Teesside katika kile shirika linalokabiliana na unyanyasaji wa wanyama nchini Uingereza RSPCA linasema ni kitendo cha ukatili.

Wanandoa wawili waliokuwa wakitembea katika eneo la Kirkleatham Wood ,walisikia kilio cha kitu kilichokuwa kikilia kwa uchungu na kumpata mbwa huyo ambaye tayari alikuwa amezikwa.

Alikimbizwa kwa daktari wa wanyama lakini majeraha yake mabaya yalimlazimu mtabibu huyo kumuua.

Shirika hilo la wanyama linasema kuwa zaidi ya mtu mmoja alihusika katika kitendo hicho.

Inspekta Nick Jones alisema: katika kipindi cha miaka kumi ambacho nimefanyia kazi RSPCA,sijawahi kuona kitu cha kuogofya na ukatili mkubwa kama huu.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: