BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHUNGAJI KANISA LA WASAABATO AFA WAKATI AKIELEKEA KATIKA MAOMBI


MCHUNGAJI wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Sirari, Tumaini Lugembe (40), amekufa baada ya kugongwa kwa nyuma na gari akiwa amepakiwa katika pikipiki akienda kwenye maombi kwenye Shule ya Sekondari Sirari.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime/Rorya, Andrew Satta amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Amesema, mchungaji Lugembe aligongwa na gari aina ya Nissan Pick Up yenye namba za usajili T907 BZC lililokuwa likiendeshwa na Joseph Nyanseso.

Lugembe alikuwa amepakiwa kwenye pikipiki yenye namba MC 713 BHF iliyokuwa ikiendeshwa na Ndege Mahende (27) akienda kwenye maombi Shule ya Sekondari Sirari na ajali ilitokea katika kitongoji cha Buriba, kata ya Sirari, karibu na Mizani ya Tanroads.

Kamanda amesema dereva Mahende wa pikipiki aliyokuwa amepanda mchungaji huyo, alijaribu kupinda barabara kuingia barabara inayoenda shule ghafla kulikuwa na gari hiyo bila kuchukua tahadhari ya kupunguza mwendo na kuwagonga kwa nyuma mwendesha pikipiki na mchungaji huyo.

"Mchungaji alirushwa na kuangukia kichwa kwenye barabara ya lami na kupoteza maisha papo hapo," amesema.

Kwa mujibu wa Kamanda Satta, dereva wa gari anashikiliwa kwa mahojiano na kisha atafikishwa mahakamani.

Mwili ulifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime na kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa maziko.

Mzee wa Kanisa hilo la SDA Sirari, Martin Mokare, alisema mchungaji huyo ataagwa kanisani hapo na atasafirishwa kwenda Ukerewe, Mwanza kwa maziko.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: