BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWAMUZI WA KATI ALIYEKUNG'UTWA NA MASHABIKI WA KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA AJIGAMBA KUWA YEYE NI KIDUME


Kocha msaidizi wa Klabu ya Mwadui, Amri Said, akizuiwa na mwamuzi wa akiba, Thomas Mkombozi katika moja ya majukumu ya mwamuzi huyo.Picha ya maktaba

LICHA ya kupata kipigo toka kwa mashabiki wa Coastal Union mwishoni mwa wiki iliyopita, mwamuzi Thomas Mkombozi amejigamba yeye ni kidume na katu hawezi kuacha taaluma yake ya kuchezesha soka kisa kipigo hicho.

Mkombozi alipigwa na mashabiki wanaodaiwa kuwa wa Coastal Union baada ya kutoa penalti kwa KMC wakati timu hizo zilipokutana katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga iliyomalizika kwa wageni kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkombozi alisema aliona kama utani wakati tukio hilo likitokea maana ghafla hali ilibadilika uwanjani hapo na mashabiki walizidi kurusha mawe kutoka jukwaani ndipo alipoamua kujihami kwa kwa kukimbia.

“Ilikuwa hatari sana nimefungua kesi ya shambulio katika Kituo cha Polisi Tanga, ingawa tayari mimi nimerejea Moshi lakini siwezi kuacha urefa kwani nina miaka 16 na nimechezesha Ligi Kuu tangu mwaka 2000 nina uzoefu wa kutosha ila kupangwa mechi za FDL lazima uwe na roho ngumu watu hawataki kufungwa mimi ni mwanamume jasiri ndiyo maana niliweza kupangua mawe na virungu vilivyorushwa kwangu,” alisema Mkombozi.

Pia Mkombozi alisema inasikitisha kuona mashabiki na viongozi hawataki kukubali matokeo ya mechi yao ila anaamini haki itatendeka kwani amewasilisha taarifa sehemu sahihi, Jeshi la Polisi na Shirikisho la Soka nchini, (TFF).

Vurugu hizo zilisababisha mwamuzi huyo kuumizwa na kupelekwa hospitali ambapo alishonwa nyuzi nne kisogoni na nyuzi moja sehemu ya usoni kutokana na mawe aliyokuwa akirushiwa na mashabiki.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama alitoa kauli ya kulaani kitendo cha mashabiki hao kumpiga mwamuzi huyo na kusema kuanzia sasa watakuwa wanasusia mechi za Coastal Union hadi hapo watakapotangaza vinginevyo.

Coastal Union ambayo ilishuka daraja msimu uliopita imekuwa na rekodi mbaya ya kuwapiga waamuzi ambapo msimu uliopita ilimpiga mwamuzi Simon Charles kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga. 


Kamati ya Saa 72 ambayo hupaswa kutoa hukumu ndani ya saa hizo hadi sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwenye kamati hiyo tangu tukio litokee.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: