BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC YAUA KIMONDO FC KIMYA KIMYA LIGI DARAJA LA KWANZA


Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Polisi Moro SC imendelea kujiimarisha ligi daraja la kwanza Tanzania bara 2016/2017 baada ya kuikung’uta Kimondo FC ya Mbeya kwa bao 3-2 katika mchezo mkali uliojaa upinzani katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Vijana hao wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Urlich Matei walilazimika kucheza soka la nguvu na maarifa zaidi na dakika 90 walifanikiwa kufunga bao la tatu na ushindi kupitia kwa mshambuliaji, Salum Kihimbwa aliyefunga kwa kichwa.

Kihimbwa alifunga bao hilo akitumia vyema uzembe wa walinzi wa Kinondo FC wa kushindwa kucheza mpira wa adhabu ndogo iliomiminwa kiufundi na nahodha wa Polisi Moro SC, Nahoda Bakari na kufunga bao hilo baada ya kuruka juu na kujaza mpira huo wavuni huku kipa, Amir Mashenzi akiwa amedua.

Mabao mengine ya Polisi Moro yalipachikwa wavuni na mshambuliaji tegemeo, Ramadhan Kapera aliyefunga mabao mawili pekee yake katika dakika ya 38 baada ya kupokea majaro ya winga, Nicolaus Kabipe huku dakika 51akifunga lingine kufuatia kazi nzuri ya Jamal Fadhil.

Kimondo FC walipata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji, Mwiga Samson dakika ya 71 huku bao la pili likitumbukizwa wavuni na Monte Mwanamtwa dakika ya 86 baada ya safu ya ulinzi ya Polisi Moro SC kujichanganya katika kuondoa hatari langoni mwao na kumtungua kirahisi kipa, Benjamin Haule.

Mchezo huo uliochezeshwa vyema na Mwamuzi Chipukizi, Liston Hiraly kutoka Dar es Salaam ambapo Polisi Moro SC imekusanya pointi tisa baada ya michezo minne wakati Kimondo FC bado ina pointi moja baada ya kucheza michezo mitatu ikipoteza miwili na kuambulia sare moja.

Akizungumza na
MTANDA BLOG mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Polisi Moro SC, John Tamba alieleza kufurahishwa na matokeo hayo pamoja na mwenendo wa timu yake katika ligi hiyo wakiwa na pointi tisa. 

Tamba alisema kuwa walipoteza mchezo ugenini dhidi ya JKT Mlale kwa kufungwa bao 1-0 na kuwaharibia hesabu zao lakini katika mchezo dhidi Kimondo vijana walirejesha morali na kuibuka na ushindi wa bao 3-2 licha ya safu ya ulinzi kucheza kwa kutofuata maelezo ya benchi la ufundi na na kuahidi kuziba kasoro zilizojitokeza katika mchezo huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: