BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USINGIZI NA FAIDA ZA KUZUIAA UGONJWA WA KIHARUSI

 
WAKATI hofu kuhusiana na maradhi ya kiharusi ikishika kasi nchini kutokana na athari zake kwa jamii, imebainika kuwa ratiba ya usingizi inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ugonjwa huo.

Ripoti ya utafiti iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa, watu wanaofanya mazoezi ya mara kwa mara na kupata usingizi wa kutosha nyakati za usiku huwa na uwezekano mdogo wa kupata kiharusi.

Watafiti wamebaini kwamba miongoni mwa takribani watu wazima 300,000 nchini Marekani, wote ambao hulala kwa masaa saba hadi nane nyakati za usiku walikutwa wakiwa na uwezekano wa chini ya asilimia 25 kupata kiharusi, kulinganisha na watu ambao hulala kwa wastani wa chini ya muda huo au kulala kwa muda mrefu zaidi.

Katika utafiti huo, imebainika kuwa hatari kubwa zaidi ya kupata kiharusi ipo kwa watu “wanaolala kwa muda mrefu zaidi”, hasa wale wanaokuwa kitandani kwa walau masaa nane kila usiku unapoingia.

Lakini watu wasiolala kiasi cha kutosha – yaani wanaolala chini ya masaa saba kila usiku unapoingia – pia walionyesha kuwa katika hatari ya kupata kiharusi.

Hata hivyo, matokeo ya utafiti huo hayathibitishi kwamba usingizi wa kutosha unaweza kuziuia kiharusi, bali ni kwamba huwa kuna uhusiano kati ya kupata muda wa kutosha wa kulala na hatari ya kupata maradhi ya kiharusi.

Hadi sasa, watafiti walisema matokeo yanabainisha umuhimu wa kulala katika kudhibiti kiharusi – jambo ambalo wengi bado hawajalifanyia kazi.

"Baadhi yetu huwa tunachukulia kulala kuwa ni kama adui (wa afya). Hilo linajitokeza katika namna tunavyofanya mambo yetu," alisema kiongozi wa utafiti huo, Azizi Seixas, wa kitengo cha Mabadiliko ya Tabia kwenye Kituo cha Afya cha Langone, jijini New York City.

Hata hivyo, Seixas alisema, kuna ushahidi unaozidi kuongezeka kwamba wakati linapokuja suala la uchaguzi wa mtindo wa maisha, usingizi wa kutosha ni "nguzo ya tatu," pamoja na mlo kamili na mazoezi ya kila siku.

Timu ya watafiti ilibaini kwamba mchsanganyiko wa tabia ya kuwa na usingizi wa kutosha na mazoezi ya kila mara ulikuwa na uhusiano mzuri na kushuka kwa hatari ya kupata kiharusi.

Seixas alikuwa amepangwa katika ratiba ya kuwasilisha matokeo ya utafiti huo kwenye mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Maradhi ya Kiharusi (ASA), mjini Los Angeles. Matokeo yanayowasilishwa kwenye mkutano yanachukuliwa kuwa ni ya awali na hivyo hayawi rasmi hadi yanapochapishwa katika majarida ya kitaaluma.

Daniel Lackland, msemaji wa ASA, alisema matokeo ya utafiti huo yanawiana na umuhimu wa kufanya mazoezi katika kuimarisha afya ya moyo – na pia yanakumbusha watu wote kwamba usingizi ni muhimu.

"Inaonekana kana kwamba usingizi wa kutosha na mazoezi huwa vina uhusiano wa moja kwa moja na hatari ya kupata kiharusi," alisema Lackland.

"Ikiwa unafanya mazoezi ya mara kwa mara, hilo ni jambo zuri – na tunalitambua hilo kwa muda mrefu," alisema. Lakini pia kuna sababu kwamba usingizi una uhusiano wa moja kwa moja na hatari ya kupata kiharusi, aliongeza Lackland, ambaye pia ni profesa wa mishipa ya fahamu kwenye Chuo Kikuu cha Tiba cha South Carolina, mjini Charleston.


"Nafikiri kwa hapa labda kuna suala muhimu la shinikizo la damu," alisema Lackland.

Alieleza kwamba bila ya kuwa na usingizi endelevu na wa kutosha – maana yake huamki usiku – kasi ya damu yako mwilini haiwezi kushuka hadi kuwa katika kiwango chake cha chini zaidi.

"Figo, moyo na ubongo hufanya kazi kidogo wakati wa kulala," alisema Lackland.
"Kama hulali vizuri, kupungua huko kwa kazi huwa hakutokei."

Seixas alikubali kwamba kutolala vya kutosha kunaweza kusababisha athari za moja kwa moja za matatizo ya moyo.
Aidha, kuhusiana na "kulala kwa muda mrefu zaidi" na namna kunavyoongeza hatari ya kupata kiharusi, Seixas alisema jambo hilo linaweza kuashiria uhusiano usiokuwa wa moja kwa moja.

"Kwa mfano, kama unalala sana, maana yake ni kwamba pengine huwa hufanyi kazi za kutosha wakati wa mchana," alisema.

Utafiti unaonyesha kwamba watu wazima wa Marekani takribani 289,000 walihusishwa. Seixas na watafiti wenzake walitumia mfumo wa kompyuta kukadiria athari za kompyuta, mazoezi na mitindo ya maisha inavyowahatarisha watu kupata kiharusi.

Kwa ujumla, "watu wanaolala sana " walikuwa na asilimia 146 zaidi ya kuumwa kiharusi, kulinganisha na washiriki wengine wote katika utafiti huo.

Aidha, watu wanaolala kwa muda mfupi, walionyesha kuwa na asilimia 22 zaidi ya kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huo wa kiharusi, kulinganisha na watu wa makundi mengine.

Seixas alisema kuna uwezekano mdogo kwa watu wanaolala vizuri kila uchao na kushiriki mazoezi kupata kiharusi – hiyo ikimaanisha kuwa ni kutumia wastani wa dakika 30 hadi 60 za mazoezi makini kama ya kukinbia, walau mara tatu hadi sita kwa wiki. Katika kundi la watu wenye sifa hizo za kulala vizuri na kushiriki mazoezi, chini ya asilimia 1.2 ndiyo hupata kiharusi.

Kuhusiana na mazoezi, Seixas alisema: "Zingatia kile unachoweza kufanya… ikiwa ni mara yako ya kwanza, anza kwa kutembea. Kutembea kuzunguka nyumba ni bora kuliko kukaa tu bila ya kufanya mazoezi." 


Vivyohivyo, Seixas alisema, ikiwa huwezi kupata muda wa kulala kwa wakati nyakati za usiku – labda kwa sababu una zamu za usiku – hakikisha kwamba unajipa muda wa kutosha wa kulala nyakati za mchana.”
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: