BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DR JOHN POMBE MAGUFULI AJIGAMBA KWA SIKU 365 TANGU AANZE KUONGOZA TANZANIA KWA CHEO CHA URAIS

Rais John Magufuli anatimiza siku 365 leo tangu alipoapishwa kushika nafasi hiyo Novemba 5, 2015 huku akiainisha mambo kadhaa ya mafanikio na mengine ya changamoto katika kipindi hicho cha kuwa madarakani.

Katika mazungumzo yake na wahariri na waandishi wa habari, Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alitumia takribani saa tatu kujibu maswali mbalimbali kabla ya kujumuika nao (wandishi) kwenye chakula cha mchana.

Katika ufafanuzi wake wakati akijibu maswali aliyoulizwa,
Rais Magufuli alieleza kuhusu mafanikio ya Serikali yake katika kutimiza ahadi ilizotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 na pia kuelezea changamoto kadhaa. 


Ununuzi wa ndege mbili na mpango wa kuongeza nyingine hadi kufikia saba kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa Shirika la Ndege (ATCL), vita dhidi ya ufisadi, kuongeza mapato kupitia makusanyo ya kodi, kutolewa kwa elimu bure.

Nyingine ni kubana matumizi yasiyo ya lazima ya serikali kwa nia ya kupeleka fedha zaidi kwenye miradi inayowagusa wananchi moja kwa moja na pia kuimarisha huduma za afya kwa kununua dawa zaidi ili kukidhi mahitaji ni miongoni mwa jitihada zenye mafanikio katika kipindi hicho cha siku 365.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment