BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MUSWADA WA HABARI WAPITA HUKU UKICHA VUMBI BUNGENI DDODOMA



Mvutano baina ya wabunge kuhusu Muswada wa Huduma za Habari wa Mwaka 2016, umetawala na kisha kupitishwa na sasa unasubiri kutiwa saini na Rais John Magufuli ili uwe sheria.

Awali, mjadala wa muswada huo ulitawaliwa na kurushiana vijembe kati ya pande mbili.

Katika mjadala wa muswada huo, mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Jamii, Peter Serukamba amesema kati ya wachangiaji, hakuna ambaye alilenga kupinga vifungu vilivyo kwenye muswada huo bali walijikita katika siasa.

“Mkitaka kujua muswada huu ni mzuri sikilizeni kuanzia jana (juzi) hadi leo (jana) hakuna mtu aliyepinga vifungu na kama yupo mtu asimame. Wote mliamua kucheza siasa tu. Lakini kwa maana ya sheria yenyewe hakuna mtu aliyeweka neno kwa sababu kila kitu kimefanywa,” amesema.

Alisema yaliyoletwa na kambi ya upinzani yote yalikuwa yameshaondolewa na wanayoyachangia hayamo katika muswada huo.

Serukamba amesema kilichokuwa kikisemwa bungeni ni kuwa wadau hawakushirikishwa, lakini kama hawakufanya hivyo ni kwa kupenda.

Mbunge wa viti maalumu (CCM), Juliana Shonza ametaka wanasiasa kuacha kuingilia utendaji wa vyombo vya habari.

Wakati Shonza akiendelea kuchangia, mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee ametamka maneno (milioni 10 hizo) jambo ambalo lilimkera Shonza na kumtolea maneno makali.

Mbunge wa Welezo (CCM), Saada Mkuya amesema kwa kawaida Serikali inapoleta miswada ya sheria, huja na uanzishwaji wa mifuko.

“Nawaomba wabunge wenzangu mbali na kukupongeza sana waziri, lakini tunakuomba utakapokuja mwaka ujao na bajeti uje na source of fund (vyanzo vya mapato),” amesema.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zainabu Vullu amesema muswada huo unakwenda kutetea masilahi ya waandishi.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema masharti ya Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 yameingizwa kama ilivyo kwenye muswada huo.

Lissu amesema sheria hiyo ilikuwa inazungumzia utoaji leseni kwa waandishi wa habari, lakini suala hilo likaondolewa kwa kuwa lilikuwa linapingana na Katiba.

Pia, amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1928 imeingizwa kama ilivyo kwenye Sheria ya Huduma za Habari, wakati ilitungwa na wakoloni kuzuia kushamiri kwa vyombo vya habari vya wazawa.

Wakati huohuo muswada huo umepita huku kukiwa na marekebisho 32 ya Serikali kati ya vifungu 67 vya muswada huo.

Awali, vifungu vilivyoingizwa bungeni vilikuwa 62 lakini Serikali ilipeleka mapendekezo kuingiza vipya. Hali ya hewa nusura ichafuke baada ya mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika kutaka kujua sababu za maoni ya wapinzani kutoingizwa, jambo lililofanya Bunge lisimame kwa dakika tano na nusu.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: