BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI ASAINI SHERIA YA HABARIRais wa Tanzania, John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge katika mkutano wake wa tano bungeni mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa ametoa taarifa na kueleza kuwa Rais Magufuli amesaini sheria hiyo Novemba 16 mwaka huu 2016 na kuwapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwake.

Novemba 4 mwaka huu Rais Magufuli katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari nchini alisema kuwa mara tu sheria hiyo itakapofikishwa kwake ataisaini mara moja. 


Rais Magufuli alisema hayo huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa habari nchini wakiomba muda kupitia sheria hiyo na kutoa maoni yao.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment