BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU ATAKA SAUTI ZA ADHANA KWA AJILI WA SWALA ZIPUNGUZWE MISIKITINI

Waziri mkuu wa Israel ametoa wito kwa wanaoita watu kwa ibada kupunguza sauti nchini humo
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaunga mkono pendekezo la kupunguza sauti za wito wa ibada 'adhan', akisema kuwa amepokea malalamishi ya kelele.

Baadaye siku ya jumapili kamati ya serikali itajadili mswada ulio na mpango huo.

Vyombo vya habari vya Israel vinasema kuwa mikakati hiyo itazuia misikiti kutotumia vipaza sauti mara tano kwa siku ili kuwaita wafuasi wa dini hiyo kufanya ibada.

Wakosoaji wanasema hatua hiyo itakuwa ya ukadamizaji.

Sheria hiyo itaathiri dini zote lakini itatumika sana miongoni mwa wito wa ibada miongoni mwa waislamu au 'adhan'.

Adhan ya kwanza hufanyika mapema alfajiri huku ya mwisho ikifanyika baada ya jua kutua.

Takriban asilimia 17.5 ya raia wanaoishi Israel ni Waarabu na wengi wao ni Waislamu.BBC
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment