BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO WA NG'OMBE ASWEKWA MAHABUSU

MFANYABIASHARA Ndama Hussein, maarufu kama ‘Mtoto wa Ng’ombe’, ameendelea kukaa rumande hadi Krismasi baada ya kesi yake ya tuhuma za kutakatisha Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh. bilioni 1.181) kuahirishwa hadi Desemba 27, mwaka huu.

Kesi hiyo ambayo Ndama anadaiwa kughushi na kutakatisha fedha, ilipangwa kutajwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa, lakini upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa, alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kutokana na ombi hilo, Hakimu Nongwa alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 27 na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.

Mapema mahakamani hapo, Msigwa alidai kuwa Februari 20, 2014, jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya, mshtakiwa alighushi nyaraka za kusafirisha madini.

Katika kufanya hivyo, alidai mshtakiwa alionyesha kuwa Kampuni ya Muru Platinum Tanzania Investment Limited imepewa kibali cha kusafirisha maboksi manne ya vipande vya dhahabu yenye uzito wa kilo 207 yakiwa na thamani ya Dola za Kimarekani 8.2 kwa Kampuni yenye makazi yake nchini Austaria, inayojulikana kama Trade TJL DTYL Limited huku akijua nyaraka hizo za uongo.

Katika shtaka la pili, Machi 6, 2014 jijini Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya, mshtakiwa aliandaa nyaraka za uongo kuonyesha kwamba hati ya kuondolea mizigo kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa za tarehe hiyo, akiwa na lengo la kuonyesha kwamba vipande vya dhahabu vyenye uzito wa kilo 207 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa zinasafirishwa na Kampuni ya Muru Platinum kwenda Austraria.

Msigwa alidai katika shtaka la tatu, Februari 20, 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa na nia ya kudanganya, alighushi nyaraka zikionyesha kuwa ni fomu ya tamko la kodi akionyesha Kampuni ya Muru Platinum imelipa Dola za Kimarekani 331,200 kama kodi ya kuingiza mzigo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kilo 207 ya vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku akijua ni uongo.

Aidha, katika shtaka la nne, Februari 20, 2014 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa na nia ya kudanganya, alitengeneza nyaraka za uongo za kuonyesha kuwa ni za bima kutoka Kampuni ya Phoenix Ltd za terehe hiyo, akilenga kuonyesha kwamba Kampuni ya
Muru Platinum imekatia bima maboksi manne ya vipande vya dhahabu zenye uzito wa kilo 207 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 huku akijua ni uongo.

Katika shtaka la tano na sita, kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014 jijini Dar es Salaam, alijipatia kwa njia ya uongo na kutakatisha
Dola za Kimarekani 540,390 (sawa na Sh. Bilioni 1.181) kutoka Kampuni ya Trade TJL DTYL Limited kwa madai kuwa angesambaza na kusafirisha nje ya nchi kilo 207 za vipande vya dhahabu vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 8,280,000 lakini hakufanya hivyo. 


Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitakatisha fedha hizo zilizopatikana kwa njia ya jinai kwa kuelekeza kiasi hicho cha fedha kuingizwa katika akaunti iliyoko benki ya Stanbic yenye jina la Kampuni ya Muru Platinum na baadaye alizitoa zote na kuzitumia kwa matumizi binafsi huku akijua zimepatikana kwa njia ya udanganyifu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: