BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAO LA MWENDO KASI LA MITA 25 LAIDIDIMIZA SIMBA SC KWA KUIKOSESHA KOMBE LA MAPINDUZI CUP 2017


Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi kombe la ubingwa wa Mapinduzi nahodha wa Azam FC, John Bocco baada ya timu hiyo kuifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa fainalijana Uwanja wa Amaan. Picha na Anthony Siame

Zanzibar. Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.

Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.

Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.

Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.

Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.

Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: