BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATU WACHANGISHWA FEDHA ILI KUCHOCHEA MGOGORO WA ARDHI LOLIONDO ARUSHA


WAKATI Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kamati zima ya wataalamu wa uhifadhi na wadau wengine, wako katika hatua ya kwanza ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo katika Pori Tengefu la Loliondo, linalomilikiwa na Kampuni ya Uwindaji ya Orttelo Business Corporation (OBC), tayari kumeanza vikao vya kupinga jitihada hizo na wananchi wanachangishwa Sh 200,000 kwa lengo la kwenda mkoani Dodoma, kumwona Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika katika Kijiji cha Oldonyowas na Olemishiri wilayani Ngorongoro, zimeeleza kuwa vikao hivyo vilihudhuriwa na baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na baadhi ya viongozi wa mila wa jamii ya Kimasai maarufu kwa jina la Laigwanani.

Vyanzo vya habari vya uhakika vilisema miongoni mwa wanasiasa waliohudhuria kikao hicho ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Mathew Siloma ambaye ni Diwani wa Kata ya Arash na Diwani wa Chadema wa Kata ya Olelerien –Magaidula (Wasso Mjini), Metui Ole Tipap.

Habari zilieleza kuwa mkutano huo uliratibiwa na kigogo mmoja wa siasa wilayani humo na baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya kufahamu ajenda za mkutano huo kwa lengo la kupambana na OBC, iliyoamua kusema ukweli juu ya mamilioni ya dola inayotoa kwa halmashauri hiyo hatua, ambayo haikuwapendeza baadhi ya viongozi wa wilaya.

Kikao hicho kiliazimia kwa kauli moja kupingana na ushauri uliotolewa na wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songoro kuwa kilimo na uchungaji vinapaswa kupigwa vita katika pori hilo la Loliondo na vyanzo vya maji vilivyopo katika pori hilo na hifadhi ya Serengeti vinapaswa kulindwa kwa nguvu zote.

Habari zilisema kuwa mbali ya hilo, maazimio mengine ni pamoja na kupinga kwa nguvu zote eneo hilo kugawa kwa kilometa za mraba 1,500 na mapito ya wanyama na jitihada hizo zinapasa msukumo na baadhi ya wanasiasa wakongwe wa wilaya na mkoa kwa maslahi yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngorongoro, Mathew Siloma alipoulizwa na mwandishi wa gazeti hili kwa njia ya simu ya kiganjani kuendesha kikao hicho, alikana kalini alikiri kuwa binafsi hakubaliani na ushauri uliotolewa na timu ya wataalamu iliyoongozwa na Profesa Songoro.

Siloma alisema ushauri huo una lengo la kuendelea kuchochea mgogoro huo, uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 na ni jambo gumu pori hilo kuendelea kuwa uhifadhi kwani vijiji vinavyozunguka pori havinufaiki.

“Binafsi siungi mkono ushauri wa Profesa Songoro na timu yake na ninaomba ulitambue hivyo wewe mwandishi,” alisema mwenyekiti huyo kwa jazba. Naye Diwani Tipap alipopigiwa simu yake ya kiganjani na kuulizwa juu ya kikao hicho na kuazimia hayo, alishindwa kukanusha wala kuthibitisha, bali alidai yuko juu ya pikipiki apewe dakika tano atakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia, lakini alipopigiwa hakupokea simu tena.

Mwaka 2009, serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iliagiza kampuni zote za uwindaji kuwa vijiji vinavyozunguka eneo la kitalu inapaswa kutoa dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 10) kwa kwa mwaka kwa ajili ya huduma za maendeleo kwa vijiji hivyo.

Kutokana na maagizo hayo ya serikali, OBC kwa mwaka kampuni hiyo hulipa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro zaidi ya Sh milioni 252 sawa na Sh milioni 31 kwa kila kijiji tangu mwaka 2006 hadi mwaka 2006 hadi sasa; huku watu wakihoji fedha zinapelekwa wapi na vijiji kulalamika kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Raphael Siumbu hakupatikana kuelezea mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo kutoka OBC.

Waziri Mkuu Majaliwa alipofanya ziara mkoani Arusha hususani wilayani Ngorongoro alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo kuhakikisha anamaliza mgogoro huo na kukaa na pande zote kwa lengo la kumaliza mgogoro huo na yeye kupata taarifa ndani ya muda mfupi ujao.

Gambo alifanya hivyo na wiki iliyopita timu ya wataalamu wa uhifadhi, wadau, viongozi wa mila na wenyeviti wa vijiji, walitembelea pori tengefu na kujionea changamoto zilizopo na kutoa ushauri katika kikao cha mwishio nini kifanyike kuondoa sitofamu ya mgogoro huo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: