BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ALIYEFUKUZWA MSUMBIJI AFARIKI DUNIA MTWARA, RAFIKI YAKE AACHIWA MTOTO

Agnes John Charles akiwa na mtoto Shadrack, ambaye mama yake Jackline Grayson alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara alipokuwa akitibiwa. Picha na Haika Kimaro

Mtwara. Jackline Grayson, ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Ligula baada ya kurudishwa nchini kutoka Msumbuji, anadaiwa kuwa na wadogo zake wawili wanaoishi Ubungo Maziwa, Dar es Salaam na kwamba ni mwenyeji wa Njombe.

“Msumbiji alikuwa anafahamika kwa jina la Jackline Grayson, lakini nimesikia jina la nyumbani kwao ni Josephine Sanga. Dar es Salaam ana wadogo zake wawili ni vyema kama wakisikia taarifa hizi (wajitokeze),” alisema Agnes John ambaye anatunza mtoto wa marehemu.

Akiwa anajipanga kuanza upya maisha, Agnes, mmoja wa Watanzania waliotimuliwa Msumbiji, anakabiliwa na mambo mawili mazito; kumpoteza rafiki yake na kusaka ndugu wa mtoto wa mwaka mmoja aliyeachiwa.

Agnes, ambaye ni mwenyeji wa Mbeya, anaishi na Watanzania wengine waliorejeshwa nchini katika mahema yaliyowekwa Uwanja wa Mashujaa mjini hapa kusubiri kupiga hatua nyingine baada ya harakati zao za kutafuta maisha Msumbiji kukatishwa ghafla.


“Siwafahamu ndugu wa marehemu,” alisema Agnes na kuongeza: “Naomba ndugu zake wajitokeze ili kumzika na kufanya uamuzi kuhusu mtoto wake.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: