ASKARI Magereza aliyefukuzwa kazi mwaka jana mwenye namba B 6034 CPL, Elia maarufu kama SGT Frank, amekamatwa na Jeshi la Polisi, akiwa amevaa sare za jeshi hilo huku akikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.
Elia alikiri mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Polisi cha Kati, kuwa alilazimika kuvaa sare hizo za jeshi hilo ili aweze kusafiri kutoka nyumbani kwake hadi mjini.
“Nilikuwa nafanya kazi Keko Magereza na niliachishwa kazi Desemba mwaka jana, nilivaa sare kwa sababu sikuwa na nauli ya kuja mjini, wito wangu naomba watu wengine wasifanye kosa hili, baada ya kutoka hapa nitakwenda kuzirudisha sare hizi kituo cha kazi nilichokuwapo awali,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema Elia wakati akisimamishwa kazi alikuwa na cheo cha Koplo, lakini walipomkamata juzi alikuwa na alama za Sajenti.
Alisema alipatikana na sare hizo kinyume cha sheria huku akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule.
Alisema upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na ukikamilika jalada litakabidhiwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
Wakati huo huo, jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watatu wa ujambazi wa kutumia silaha.
Sirro alisema watuhumwa hao walikamatwa juzi eneo la Kivule wakiwa kwenye kikao chao cha kupanga kufanya uhalifu.
Alisema katika mahojiano watuhumiwa hao ambao ni Justine Masiko maarufu kama Yassin Masiko, Alex Sirari na George Maximillian Jiabe walikiri kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha jijini Dar es Salaam na mikoani.
Katika hatua nyingine, Sirro alisema kikosi cha Usalama Barabarani Kanda hiyo, kimevunja rekodi kwa kukusanya zaidi ya Sh. milioni 218 ndani ya siku mbili, fedha zinazotokana na makosa ya usalama barabarani. Alisema tatizo kubwa la makosa ya barabarani ni ulevi na watu kutofuata sheria.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ ASKARI MAGEREZA ALIYEFUKUZWA KAZI NAMNA ALIVYOTUMIA SARE ZA JESHI HILO KUKWEPA NAULI KATIKA DALADALA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment