BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAISHA YA NUNGUNUNGU NA NAMNA ALIVYOZUNGUKWA NA MAADUI KILA KONA

 Nungunungu au nungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadu. Wadadisi wanasema kwamba miiba hii hufikia hadi 30,000 akiwa mkubwa

Kwa kipindi kirefu nungu huaminika kuwa na uwezo wa kurusha miiba yao kwa adui, hii imekanushwa vikali, baada ya kufahamu kuwa miiba hulegea na kuanguka yenyewe.

Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba, vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. 


Nungu huweza kupatikana hata kwenye miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungu ni wanyama wanaopiga kazi usiku na mchana hulala.

Ni vigumu sana kuweza kuwaona kwa vile wanaishi kwa mashaka sana maana mara tu wanapoonekana machoni pa watu hushambuliwa na kuwaua kwa sababu mbalimbali.


Wengine huwaua kwa sababu ya kuwatuhumu kuwa wanakula mazao yao mashambani lakini wengine huwaua kwa sababu wanadai kuwa miiba yake ni dawa.

Katika Tanzania inasemekana Nungunungu hupatikana kwa wingi katika mapori mbalimbali likiwemo pori la Nyamunsi lililoko Wilayani Tarime Mkoa wa Mara.


Baadhi ya Wenyeji wa sehemu hiyo wanaamini kuwa ngozi ya Nungunungu ni dawa ya watoto wadogo na hivyo waganga wengi huwawinda na kuwatumia kwa lengo la kutibu watu kutokana na imani tofauti katia jamii.

Pia Nungunungu anahusishwa sana na uchawi kwani anaaminika kuwa ukimkuta njiani ni ishara ya kutokea kwa jambo fulani baya au zuri.

Ni jukumu la sisi Watanzania kuhifadhi makazi ya wanyamapori kwa kuwa ni suala la sisi sote.


Wanyamapori hawa ni urithi wetu, kila mmoja wetu atimize wajibu wake kwa nafasi yake ili kuhakikisha huo ni rasilimali ya wanyamapori na matumizi yake vinakuwa enendelevu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: