BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAJI MANARA WA SIMBA SC AIVURUGA KAMATI YA KATIBA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI


UONGOZI wa klabu ya Simba umesema hakukuwa na haja ya Kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za wachezaji kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili marejeo (Review) ya shauri la timu ya Kagera Sugar kwa madai kuwa haina uhalali huo.

Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Kamati hiyo kukutana juzi kwenye Hotel ya Protea kupitia shauri hilo ambapo mpaka sasa bado maamuzi yake hayajatangazwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa klabu ya Simba SC, Hajji Manara aliwaeleza kuwa licha ya kutokuwa sahihi kwa Kamati hiyo kuketi kwakua suala hilo lilitakiwa lipelekwe bodi ya ligi lakini pia kwa mujibu wa sheria za nchi shauri la mrejeo halipaswi kufanyika kwa kuita mashahidi wapya kama ilivyotokea.

“Licha ya kikao kutokuwa sahihi lakini pia kwenye suala la Review hakupaswi kuitwa mashahidi wapya sasa nashangaa kuna waliohojiwa ambao katika maamuzi ya awali hawakuwepo.

“Haijawahi kutokea duniani kote kuwa mtuhumiwa anaitwa kwenye Review au mwamuzi wa nne (Fouth Official) ambaye hata haandiki ripoti anaitwa kutoa ushahidi kwenye kamati jambo ambalo halijawahi kutokea,” alisema Manara.

Manara alienda mbali kuwa endapo watashindwa kupata haki yao suala hilo litafika mbali kwa maelezo kuwa wamechoka kuonewa na TFF ambao mara nyingi wamekuwa wakiipendelea Yanga.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: