BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MACHACHE ZAIDI KUHUSU KOREA KASKAZINI

Nchi ya Korea Kaskazini imehalisha kilimo cha bangi na haichukuliwi kama ni madawa ya kulewesha kwa taifa hilo linaloongozwa na rais Kim Jong-un.

Nchi hiyo ndio nchi pekee duniani hadi sasa amabayo imewahi kuiteka meli ya kivita ya Marekani
Geofrey Chambua anasimulia.

Wakati dunia nzima leo ni 2017 kwao ni mwaka 106 wakihesabu kuanzia kifo cha kiongozi wao Kim il-Sung-.Baba wa taifa lao Kim II-Sung aliyezaliwa April 15 mwaka 1912 ambapo ndio siku iliyozama meli ya Titanic. (Rais wa Maisha wa Korea Kaskazini ni Kim Il Sung.


Mtoto wake na mjukuu wake wamekuja kuwa viongozi tu lakini babu yao mwenyewe babu ndiye rais mpaka leo, hata kama amefariki hayo ndio mambo ya Korea. Kusini ya kuyatambua.

Hiyo siku ndio chanzo cha kalenda yao (Democratic People's Republic of Korea_Juche Korea[/QUOTE] year Gregorian year Dangun year-Kim alizaliwa 1912 ~ hapa ndio juche year inaanzia)

Kuanzia mwaka 2009 nchi hiyo siyo ya kikomunist tena na wana msimamo au Ideology yao mpya unaitwa "JUCHE" wakimaanisha "KUJITEGEMEA"

Kosera Kaskazini ndio nchi yenye uwanja mkubwa wa mpira kuliko yote dunia nzima ambao unaingia na kuketi kwenye viti watu 150,000 kwa wakati mmoja.
 

Miaka ya 50, Korea Kaskazini walijenga mji Fake (Nice City) mpakani ili kuwavutia watu wahamie kutoka South Korea.

Korea Kaskazini kuna mitindo 28 tu ya nywele iliyohalalishwa na serikali, 10 kwa wanaume na 18 kwa wanawake na kama mtu anataka kusuka ama kunyoa atachagua kutoka mitindo iliyopitishwa na serikali hiyo na anayekaidi anachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kwa miaka ya 60 iliyopita ni wakorea kaskazini 23,000 waliokimbilia Korea Kusini wakati ni wakorea kusini wawili tu ndio wamerudi Korea Kaskazini.(Christian Amanpour wa CNN like 3 years ago alifanikiwa kupata visa ya kwenda North Korea na alisema imemchukua 10 kuipata hiyo visa!!!)

Wakati dunia nzima inatumia OS za Windows, Linux au Mac OS etc , wao wanatumia windows ya kwao inayoitwa Star OS.

Korea Kuskazini kumiliki binlia, Kuangalia movie au tamthilia za Korea Kusini na kusambaza picha za ngono adhabu yake ni kifo endapo utabainika na vyombo vya dola na katiba yao inaweka uhuru wa kuabudu (but in reality) hicho kitu hakipo na kama utaona watu wanasali kidogo huwa ni watalii wenye dini zao au mabalozi kuwaridhisha.



Kuna gereza maalumu kwa watu wenye kutaka ukristo lipo kanisa ufu Chung chang Catholic Cathedral lililjengwa na Serikali na yasemekana kuna maandamo ya siri kudai Ukristo.

Wanajeshi na viongozi wa serikali ndio wanaruhusiwa kumiliki gari zaidi ya hapo ni tatizo na ni kinyume cha sheria kuvaa jeans Korea Kaskazini na ni marufuku kuvaa jeans hasa za rangi ya blue na ukikutwa umevaa ni kwenda jela au kunyongwa sababu unaeneza tamaduni za adui yao Marekani.

Korea Kusini hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano lakini sanduku la kura ni moja tu na mgombea ni mmoja.

Kuna Shirika Linalotumia parachuti kuzipeleka BIBILIA nchini humo wakiomba angalau ziangukie kwa mmoja aelewe neno.

Kulingana na vitabu vya nchi hiyo Kiongozi wao Kim Jong Un alijifunza kuendesha gari akiwa na miaka mitatu tangu azaliwe.

Hasara ama maudhi wanayoyapata wananchi waliozaliwa tarehe 8 July au tarehe 17 December. waliozaliwa tarehe hizo waruhusiwi kusherekea ya kuzaliwa (Birthday) maana siku hizo ndizo viongozi wao Kim Jong Il na Kim Il song walifariki dunia.

Wanamiliki kikosi maalumu cha wanajeshi wenye akili sana/geneus kama jeshi la kimtandao,Special cyber hackers, Unit 121 au Beaureu 121. Na inasemekana wametuma baadhi yao zaidi ya askari hao 1200 nchi mbalimbali kwa mashambulizi au cyber war. Ndio waliohusika katika Shambulizi la Kampuni ya SONY kulingana na vyombo vya magharibi.
 

Mkorea Kaskazini haongei Kiingereza kabisa lakini bado ametengeneza software yake yeye mwenyewe yaani hatumii windows, hivi sasa wametengeneza smart phone yao isiyotumia android yaani wamebuni software ya kwao.


Kuna kijana mdogo mkorea kaskazini anaishi USA alipoenda NK baada ya siku kadhaa alipatikana na simu ya camera made in South Korea...sumsung alikuhumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kazi ngumu..Mataifa makubwa yalipoingilia kati aliachiwa huru na kurudishwa USA..ingawaje yeye ni raia wa korea kaskazini.

Mwaka 2015 Korea kaskazini walibadili mtindo wao wa saa, dakika 30 nyuma.Lengo lilikuwa kukwepa kuwa na saa sawa na watani wao wa Korea kusini.
 


Mgao wa umeme ni jambo la kawaida sana Korea kaskazini. Ifikapo usiku serikali huzima umeme maeneo mengi kwa sababu ya uzalishaji wake kuwa wa kiwango cha chini.
 

Channel za TV zinazo ruhusiwa kuoneshwa nchini kwao ni tatu tu.Moja kila jioni tu, na hizo mbili ni weekend pekee, zote lazima zikaguliwe na serikali kabla ya kupaa hewani.
 

Baadhi ya makosa hukumu zake hudumu kwa vizazi vitatu, siyo ajabu kwa mtu kutumikia hukumu ya makosa ya Babu yake.
 

Rais wa kwanza Kim Jong iL alipendelea sana kula Nyama ya Punda na Kunyoa Panki, ni Rais katili asiye na huruma hata chembe na sasa mwanae Rais Kim Jong Un anafuata nyayo za Baba yake naye hupenda kunyoa Panki, kula nyama ya Punda na kuua wapinzani wake.

Haikuwa kazi kubwa kuamuru mjomba wake auawe kikatili kwa kushambuliwa na kundi kubwa la mbwa wenye njaa kali ambapo matukio kama hayo yaliwahi kufanywa na Baba yake, Kim Jong Un ambaye ni muoga kusafiri nje ya nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wake.
 

Inasemekana 60% ya Bajeti ya nchi hiyo inaenda jeshini yote na raia wa taifa hilo hawaruhusiwi kufanya mawasiliano ya Simu Au Email nje ya nchi yao na mshirika kubwa wa taifa hilo ni Uchina na Urusi pekee.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: