BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AWATIMUA WATUMISHI 9,000 WENYE VYETI FEK

Rais John Magufuli akikata utepe kuangalia orodha ya majina awamu ya kwanza ya Watumishi wasio na sifa. 

RAIS Dk. John Magufuli amekabidhiwa rasmi taarifa ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma huku akiamuru watumishi 9,932 waliobainika kuwa na vyeti feki waondolewe mara moja kwenye ajira na mshahara wao wa mwezi Aprili wasilipwe.

Amesema hayo leo mjini Dodoma baada ya kukabidhiwa taarifa hiyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki katika hafla ambayo pia imehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri na viongozi mbalimbali.

Dk. Magufuli akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo alisema watumishi wengine 1,538 ambao katika ukaguzi huo wamebainika vyeti vyao vina utata wasilipwe mshahara wa mwezi Aprili.

Awali Waziri Kairuki alimweleza Rais kuwa uhakiki huo umefanyika kwa jumla ya watumishi wa umma 400,035 wa mamlaka za serikali za mitaa, taasisi na mashirika ya umma na serikali kuu.

Hata hivyo, alisema uhakiki huo haujawahusisha viongozi wa kisiasa ambao ni mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge na madini kwa sababu ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa viongozi hao sifa yao inatakiwa wajue kusoma na kuandika.Nipashe
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment