BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIONGOZI WA CUF WATAJWA KULIPUA BOMU KWENYE NYUMBA YA KAMISHNA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR


SERIKALI imesema tukio la nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu uchunguzi umebaini lilifanywa na baadhi ya viongozi wandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF).

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni amelieleza Bunge leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando, Othman Omar Haji.

“Uhalifu wowote utakaofanywa na chama chochote cha siasa au mwanachama serikali lazima ichukue hatua, hata katika suala la nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar kulipuliwa na bomu viongozi wandamizi wa CUF ndio walirusha bomu hilo,”alisema.

Masauni alisema baada ya kukamilika uchunguzi wa tukio hilo, taratibu zinaandaliwa kwa ajili ya kuwafikisha wahusika mahakamani. 


Hata hivyo, Masauni hakuwataja majina viongozi wa CUF wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo na Nipashe Digita inaendelea kufuatilia suala hilo kwa undani.Tukio la kulipuliwa nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar lilitokea Machi mwaka jana.Nipashe
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment