BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYAKAZI 2.3 MIL HUPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA AJALI SEHEMU ZAO ZA KAZI



Afisa Habari Shirika la Kazi Dunia (ILO) Tanzania, Magnus Minja akiwa na Afisa Habari Kituo cha Habari cha Umoja wa Kimataifa (UNIC),Stella Vuzo.

SHIRIKA la Kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki limesema takribani wafanyakazi milioni 2.3 wanapoteza maisha kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kutokana na ajali wanazokutana nazo mahala pa kazi.

Mwakilishi wa ILO Kanda ya Afrika Mashariki, Magnus Minja, amesema takwimu hizo ni sawa na kusema mfanyakazi mmoja hupoteza maisha kila baada ya sekunde 15.

Amesema masuala ya ajali kazini yasichukuliwe kama mambo ya kawaida na la kufanyia mzaha bali ni suala la kuvalia njuga na kuhakikisha nchini inazuia matukio ya vifo vya wafanyakazi mahala pa kazi.

Minja amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha siku ya usalama mahala pa kazi dunia lakini kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa takwimu sahihi za ajali na matukio ya vifo vinavyotokea sehemu za kazi.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: