BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAJAJ NA BODABODA ZAANDALIWA MKAKATI WA KUWABANA, 1954 WAPOTEZA MAISHA 2015 HADI 2017

Bunge limeelezwa kuwa katika kipindi cha miaka mitatu jumla watu 1,945 wamefariki dunia katika ajali za bodaboda 5,418 tangu mwaka 2015 hadi Februari mwaka 2017.

Hayo yalibainishwa jana Bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kaliua(CUF), Magdalena Sakaya.

Sakaya alitaka kujua ni ajali ngapi za bodaboda zimetokea kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 mpaka 2017 na watu wangapi wamepoteza maisha kwenye ajali hizo na walemavu ni wangapi.

Nchemba alisema ajali hizo zimesababisha majeruhi na walemavu 4,696 na kutaja mikakati ya kupitishwa kwa kanuni ya leseni za pikipiki za kubeba abiria mwaka 2009, kutoa elimu ya usalama barabarani mashulenajali hizo zimesababisha majeruhi na walemavu 4,696 na kupitia vipindi vya radio, televisheni na vipeperushi.

Alisema kati ya mikakati hiyo ni kupitishwa kwa kanuni ya leseni ya pikipiki na bajaji pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni pamoja na vyombo vya habari.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: