BannerFans.com

SUZAN KIWANGA, LIJUALIKALI WAONJA JOTO YA JIWE MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

MAJI YA MAFURIKO YASOMBA GARI LA MWANANCHI TANGA


Picha kwa hisani ya Abdallah Hamisi

Tanga.
Gari la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd (MCL) limesombwa na maji katika eneo la Mazinde, Lushoto wakati likiwa katika safari ya kupeleka magazeti mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo.

Akizungumzia tukio hilo leo asubuhi, Ofisa Usafirishaji wa kampuni ya MCL, Phillip Ringo amesema gari hilo lilisombwa na maji muda wa saa 12 asubuhi.

“Magazeti yote yaliyokuwamo ndani ya gari yameharibika, hayafai kwa hiyo kuna shida kubwa kwa gazeti letu leo mkoani humo leo,” alisema

Magari mengine manne yalisombwa na maji katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa dereva wa MCL, Mohamed Khatibu, amesema gari hilo lilikwama katika mto na likaserereka na kuingia katika mtaro wa maji.

“Tulisimamishwa eneo la Mkumbara saa kumi alfajiri baada ya askari wa usalama barabarani kuyasimamisha magari yote yasipite eneo hilo. Lakini baada ya kuruhusiwa saa 12 asubuhi tukasombwa hapo Mazinde,” amesema na kuongeza

“Tupo salama hapa lakini magazeti yamelowa maji, askari wako kwenye eneo hili kusaidia."Mwananchi
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads