BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MKUU AHITIMU ELIMU YA DARASA LA 12 AKIWA GEREZANI KUTUMIKIA KIFUNGO

Waziri wa zamani ambaye anatumikia kifungo gerezaji baada ya kupatikana na kosa la kula rushwa amefaulu mtihani wa kumaliza shule India akiwa na miaka 82.

Om Prakash Chautala, aliyehudumu kama waziri mkuu wa jimbo la Haryana kaskazini mwa India kwa mihula minne, alifanya mtihani wa darasa la 12 akiwa katika jela ya Tihar mjini Delhi.

Mwanawe wa kiume Abhay Chautala alisema babake aliamua "kutumia vyema muda wake gerezani".

OP Chautala alipatikana na makosa kuhusiana na kuajiriwa kwa walimu.

Abhay Chautala aliambia gazeti la Indian Express kwamba babake amekuwa kila siku akienda kusoma katika maktaba ya gereza hilo.

"Husoma magazeti na vitabu. Huwa anawaomba wafanyakazi wa jela kumtafutia vitabu avipendavyo zaidi. Husoma vitabu kuhusu wanasiasa maarufu duniani,2 amesema.

Bw Chautala na 54 wengine, walipatikana na hatia ya kughushi vyeti walipokuwa wanwaajiri walimu 3,206 kati ya 1999 na 2000.

Waendeshaji mashtaka walisema watu waliokuwa wamehitimu zaidi walikataliwa na badala yake wale waliokuwa wametoa hongo wakaajiriwa.

Bw Chautala ni kiongozi wa chama cha Indian National Lok Dal Party na ni mwana wa aliyekuwa naibu waziri mkuu Devi Lal.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: