BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AZINDUA DAWA YA WAFANYABIASHARA WAKWEPA KODI


Rais Dk John Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua mfumo wa ulipaji kodi kielektroniki jijini Dar es Salaam leo.

RAIS Dk John Magufuli amesema Serikali imejenga kituo cha Data Centre (mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki) kwa lengo la kudhibiti ukwepaji kodi na kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano Tanzania katika kujenga uchumi.

Rais ameyasema hayo leo wakati akizindua mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki jijini Dar es Salaam ambapo Rais, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar walipewa Ipad maalum zitakazowawezesha kufuatilia ulipaji kodi utakavyokuwa ukifanyika.

Katika hotuba yake Rais Magufuli alisema kuna wafanyabiashara ambao sio waaminifu na kusema uongo kuwa wanapata kipato kidogo kwa lengo la kulipa kodi kidogo, ilhali wanapata kipato kikubwa na kuamua kuiibia serikali kwa makusudi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wote hao dawa yao ni Data Center (Kituo cha ulipaji kodi kielekroniki) ambao hawatakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipa kodi kwa wakati na kwa kiwango stahili.

Amesema anapenda sana ubinafsishaji kwa ujumla na kuwaomba wananchi wasimuelewe vibaya kuhusu ubinafsishaji "Watu wasinielewe vibaya kuwa nachukia ubinafsishaji, lakini ubinafsishaji wa hovyo nauchukia kwelikweli” amesema Dk Magufuli kwa msisitizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: