BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

EDWARD LOWASSA MIKONONI MWA POLISI TENA



Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili leo, Julai 20 saa mbili asubuhi makao makuu ya Jeshi la Polisi kwenye ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Lowassa ameambatana na mkewe, Regina na mwanasheria wake, Peter Kibatala.

Hii ni mara ya nne kwa Lowassa kuripoti hapo akituhumiwa kutoa kauli za kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23, na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa gerezani akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili waachiwe huru. Polisi wameimarisha ulinzi eneo hilo, huku Lowassa akiwa ndani tayari kwa kuhojiwa.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: