BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO NDANI YA JESHI LA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro

Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ndani ya jeshi hilo.

Katika mabadiliko hayo, Kamanda Sirro amemteua aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Julai 18 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnaba Mwakalukwa, imeeleza kuwa nafasi ya Kaganda imechukuliwa na Kamishna Murilo Jumanne.

Kabla ya hapo, Kamanda Jumanne alikuwa Kamanda wa Polisi, mkoa wa Shinyanga.

“Nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Jumanne, Shinyanga, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP) Simon Sylverius ambaye alikuwa Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Mara,” amesema. 


Taarifa hiyo imesema, mabadiliko hayo ni ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi na utendaji wa kazi.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: