BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUIPER OOT CLOUDS NI VIUMBE HATARI WANAOPANGA KUWAANGAMIZA BINADAMU HAPA DUNIANI

 

Na Geofrey Chambua.
Nyuma ya Kuiper Belt kuna kitu kingine kinaitwa Oort Cloud,hii ni aina nyingine ya mkusanyiko mkubwa sana wa vitu vinavyoelea angani vilivyofanya mkusanyiko wa aina yake.Eneo hili liko mbali sana na eneo la jua letu (Our solor system).

Vitu vinavyotengeneza mkusanyiko huu vinafanana na vile vinavyotengeneza mkusanyiko wa Kuiper Belt.Maeneo yote mawili yana mambo yanayofanana kwa namna fulani na ndiyo sababu ya kuandika makala hii kwa siku ya leo ili tujaribu kutafakari kuhusu maeneo haya.

Kutokana na tabia na maelezo yanayohusu maeneo haya ni watu wachache sana wanaofahamu kuyahusu,lakini pia kuna maelezo ambayo hayaeleweki sana kuyahusu.


Mfano wataalam wa anga wanasema kwamba Kuiper Belt itatoweka baada ya miaka 100 ijayo,hapo hapo tunaelezwa kuwa Kuiper Belt iko pale kwa mabilioni ya miaka,sasa ni kitu gani kinasababisha mkanda huu uondoke baada ya miaka 100 wakati uko pale kwa billions of years?.

Swali hili halijaweza kujibiwa ipaswavyo na siyo swali hili tu bali na maswali mengine kama vile sababu ya kuonekana kuna uwezekano wa kuwepo kwa uhai kwenye eneo hilo kwasababu vitu kama mawe madogo na makubwa sana yanayounda maeneo yote mawili ya Kuiper Belt na Oort Cloud yanaonekana yana barafu na sote tunajua kuwa barafu ni maji na sehemu yoyote yenye maji basi kuna uhai....

Kama wale wataalamu wa mambo ya Intelligence wanavyoelewa ni kwamba mara nyingi mahali ambapo kunapokuwa na maelezo yasiyoeleweka au yasiyoshiba na mara nyingi kunakuwepo na hali ya kuficha mambo au jambo.


Baada ya watu kutokuridhika na maelezo ambayo wamekuwa wakipewa kuhusiana na maeneo haya mawili,kundi la wataalamu wa anga waliamua kufanya utafiti zaidi ili kujua ni kwa nini maelezo yanapwaya.

Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu walikuja na dhana ambayo iliwastua watu wengi sana na kupelekea kuzusha mjadala mkubwa sana juu ya maeneo hayo na usalama wa binadamu hapa duniani.


Wataalam hao walikuja na maelezo kuwa maeneo hayo yote mawili yamekuwa yakitumiwa na viumbe ambao wengi wamekuwa wakiwafahamu kama Aliens na viumbe tofauti na hao.

Maelezo haya yalipingwa sana na wanasayansi na wataalam wa anga wa NASA.Pia hata wataalam wengine nao walipinga kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa uwepo wa hawa viumbe huko kwenye haya maeneo haya.

Kabla ya kuendelea sana nadhani wengi wetu tunafahamu kwamba kwenye galaxy yetu tuna nyota zaidi ya bilioni 100,na kuna bilioni zaidi ya 100 ya galaxy kwenye ulimwengu [univarse] wote.Kwa hiyo unaweza kupiga hesabu kuna nyota ngapi kwenye ulimwengu wote.


Ni nyingi sana bila shaka.Wataalam hawa wanasema kwamba,ukiacha kwenye maeneo mawili haya ya Kuiper belt na Oort Cloud, wanaamini kwamba kuna maisha pia kwenye nyota zote hizo ambazo idadi yake ni nyingi sana tena ya kutisha na kote huko kuna viumbe na viumbe hao wana uwezo mkubwa sana na mbali sana kuliko binadamu.

Tuachane na maeneo mengine na turudi sasa kwenye Kuiper Belt na Oort Cloud ambako ndiyo mada yetu ya leo na tunajadili kuhusu aina ya viumbe ambavyo wataalam hawa wamesema vinapatikana humo.

Wataalam hawa wamesema kuwa maeneo haya yanakaliwa na Aliens wa aina zaidi ya 104 na hapa nitakueleza aina chache tu.


Mtafiti wa masuala ya Aliens Stewat Swardlow, Steve Qyle na wengine wengi wamewahi kushuhudia kwa nyakati tofauti nyaraka za siri kutoka kwenye serikali tofauti tofauti kubwa duniani kama vile Marekani,China,Urusi,Japan,Ujerumani na nyingine zikionesha ukweli wa uwepo wa viumbe hawa.

Zifuatazo ni 4 kuu na kubwa za Aliens wanaopatikana kwenye mkanda wa Kuiper Belt...

1;Insectoid Aliens
2;Grey Aliens
3;Humanoid Aliens
4;Reptoid Aliens

Aina hizi ndizo ambazo serikali nyingi za dunia zimekubaliana na uwepo wake,lakini kwa siri kwasababu ndiyo aina ya Aliens ambayo imewahi kuonekana hapa duniani.


Lakini tujue kwamba,kama nilivyosema hapo juu ni kwamba wataalamu hawa wanasema kwamba kwenye mkanda wa Kuiper kuna mamia ya aina za Aliens lakini wanasema kwamba Aliens aina ya Insectoid ndiyo super power huko...

Insectoid wanadaiwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuweza kuiongoza au kuirrubuni akili ya kiumbe mwingine afikiri kama atakavyo yeye na hii ndiyo imefanya wakawa na nguvu sana eneo hilo ambalo limezua mjadala na vurugu sana baina ya wataalam wengi.Kwa maana hiyo Insectoid ndiyo aina bora zaidi ya Aliens inayopatikana eneo hilo.

Hawa viumbe ni hatari sana kwa maisha ya binadamu na karibia kila kundi la Aliens lina ajenda yake kuhusiana na binadamu na dunia hii.Kama nilivyosema kuwa kuna aina nyingi ya Aliens,hapa nitaeleza makundi machache ya Aliens na ajenda zao dhidi ya dunia na sisi wakaazi wake....

Mantids Aliens
Hawa wao wanadai kuwa dunia hii ni yao na waliishi hapa kwa miaka mingi kisha wakaondoka kwenda kutafuta maisha maeneo mengine na sasa wanahitaji kurudi.

Lionestic being Aliens
Hawa wanafanana sana na binadamu lakini pia wanafanana na Simba.


Nimekosa picha ya kuonesha namna wanavyoonekana lakini inastaajabisha sana.Hawa lengo lao ni kuondoa mtindo wa kisiasa ulioko hapa duniani.Hawa wao watasubiri hadi tumeshamalizana sana na ndipo watakuja na kuondoa kabisa mtindo huu wa siasa ulioko hapa duniani....

Humanoid Aliens
Hawa ni miongoni mwa Aliens wengi na wenye uwezo mkubwa sana na wa hatari.Inadaiwa kwamba miongoni mwa aina za hawa humanoid Aliens ipo aina ambayo inafanana kabisa na binadamu na unaweza kukaa naye kwenye kiti na usijue kama siyo binadamu.


Hawa wanaamini kuwa dunia hii iko chini ya mamlaka yao na ni eneo lao.Wanataka kuisafisha dunia yote na kuhakikisha hakuna binadamu anabakia hapa.

Wanaamini wana haki ya kufanya yote na chochote watakacho na ajenda yao kubwa ni kuondoa binadamu kwa kuwamaliza hapa duniani.Kwa mujibu wao ni kwamba binadamu ni jamii isiyokuwa halisi hivyo haistahili kuwepo kwasababu ni hatari kwa jamii hii kuendelea kuwepo.

Kwa ufupi sana hao ndiyo Aliens walioko maeneo hayo na ajenda yao kutuhusu kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbali mbali.Lakini kuna jambo lingine kutoka Japan...

Princess Kaoru Nakamaru

Picha ya tatu ni Princess Kaoru Nakamaru kushoto akiwa na Miriam Delicado walipokutana mwaka 2009 kwa mahojiano...

Huyu ni binti kutoka familia ya kifalme ya Japan ambaye aliwahi kusema kwamba amewahi kusafiri sana maeneo mbali mbali huko angani akiwa na Aliens.


Miongoni mwa mambo ambayo amesema kwamba anatamani sana kuyasema ni ukweli kuhusu historia ya kweli ya Japan ambayo anasema inakwenda hadi kwenye Israel ya kale.miongoni mwa taarifa za kustua sana ni kwamba baadhi ya maelezo yanaonesha kwamba Aliens ni wa kuwa nao makini sana maana wakati mwingine wanaweza kutumia binadamu kama chakula....

Aliens hawasemi kwa kutamka kama sisi bali wao huwasiliana kwa kusoma mawazo yako na ya Aliens wenzao tu.Wana uwezo mkubwa sana wa kufanya hivyo hivyo hawahitaji sauti ili waweze kuelewa unataka kufanya nini dhidi yao au katika mazingira uliyopo.

Huyo ndiye Princess Kaoru Nakamaru...

Je yote hii maana yake ni nini?
Ninatambua uwepo wa watu wenye msimamo kuwa masuala mazina ya Aliens ni hadithi za kufikirika na ni upuuzi tu.


Ninafahamu pia wale ambao wana misimamo kuwa Aliens wapo lakini kila mmoja ana msimamo wake kulingana na kiwango cha taarifa alicho nacho,hivyo wapo ambao wanaufahamu mkubwa sana,wengine kiasi na wengine mdogo...

Yote hayo yanakuja kutokana na aina ya maisha tuliyonayo.Kimsingi kila mmoja wetu ana haki ya kufikiri na kukubaliana vyote ambavyo anaamua kukubaliana nayo lakini ukweli na uhalisia unaweza kuwa kinyume kabisa na namna ambayo sisi au mimi nimeamua kukubali.


Unaweza kudhani kuwa uwepo wa Aliens ni upuuzi na ujinga kwasababu ni hadithi lakini hilo halitaweza kuondoa ukweli kuwa wapo,kama kweli wapo.Kitendo cha wewe kukubali uwepo wa Aliens bila kujali kiwango cha wewe kuwajua hakuwezi kuwafanya wakawepo,kama kweli hawapo...

Wewe unafikiria nini?.

Aliens ni hoax?
Kuiper Belt ni hoax?
Au Aliens wapo lakini hakuna Kuiper Belt?
Au kuna Kuiper Belt lakini hakuna Aliens?

Lakini kuna "ushahidi" wa uwepo wa Kuiper Belt lakini pia kuna "ushahidi" wa uwepo wa Aliens...

Sasa je ni nini cha kufanya?

Mawazo na mtazamo wangu.
Hapo juu nimeelezea matokeo ya utafiti wa maeneo ambayo yapo angani ambayo mimi na wengi wanaosoma hapa hatuna uwezo wa kwenda huko tukadhibitishe.


Lakini hilo halitufanyi tukatae au tukubaliane tu kirahisi tunahitaji tufanye jambo zaidi na jambo hili ni kufikiri na kutafakari [reasoning] ili tuone kama yanaleta mantiki haya yote....

Kwa miaka kadhaa kumekuwepo na taarifa za kitengo cha sayansi za anga cha Marekani maarufu kama NASA kukubali uwezekano wa uwepo wa viumbe wa ajabu huko angani.Lakini si hivyo tu kule Marekani kuna sheria inayohusiana na kuelekeza kuhusu mawasiliano baina ya raia wa Marekani na viumbe wa angani huko ambayo ni Title 14, Section 1211....

Sheria hii inazungumzia kuhusu masuala haya ya kuwasiliana na hawa viumbe..

Kwa namna ya kawaida kabisa,ni jambo lisilowezekanika mambo haya yakawa ni hadithi halafu kukawa na matukio kama haya.....

Lakini sio hayo tu.Hapo juu tumeona baadhi ya ajenda mbali mbali za hao Aliens ambazo ni kuwaondoa binadamu katika dunia hii kwa kuwaangamiza.


Kwa sisi ambao tunafuatilia mambo nje ya yale ambayo yamekuwa yakitangazwa tunafahamu sana vita iliyopo baina ya kundi moja dogo na kundi kubwa sana la binadamu kwa kundi dogo kutengeneza namna mbali mbali za kupunguza idadi ya binadamu hapa duniani.

Kama siyo kumuondoa kabisa kwa kutengeneza maradhi fake na kuleta tiba ya maradhi hayo ambayo ni ya kumuangamiza huyu huyu binadamu.Jambo hili linafanana sana na ajenda za hao Aliens kama zilivyoelezwa na watafiti.

Ieleweke kwamba kwangu mimi ni kweli kabisa kuna kundi moja la watu ambalo linatengeneza dawa,maradhi na mtindo wa maisha ambao utamuangamiza kabisa huyu binadamu.


Sijui kama ni hao Aliens aina ya Humanoid ndiyo wanafanya haya kwasababu tumeambiwa hapo juu kuna wengine unaweza kukaa nao na usijue,lakini kutokana na ajenda yao naweza kuunganisha dots na kuona kuna ka ukweli fulani hivi kwenye hili maana kuna mfanano wa mambo....

Yote katika yote,sijui kama ni kweli jambo hili liko hivi,inawezekana kukawa hakuna ukweli wote lakini nina uhakika hakuna uwongo wote hii ina maana kuna ukweli mkubwa tu pia,lakini kwangu mimi ni kwamba Aliens wapo na wapo hapa hapa duniani na pia wanahusika sana na maendeleo ya teknolojia iliyopo sasa hivi.


Nitakuja kusema siku nyingine kuhusu maendeleo ya teknolojia yaliyopo hapa duniani na kule inakotoka lakini kwa leo niseme tu kuwa kuna mahusiano makubwa sana na jambo hili na maendeleo ya kiteknolojia tuliyonayo binadamu hapa duniani....

Binadamu leo ni kama watumwa.Kuna kundi la viumbe linamuendesha sana binadamu kuanzia namna anavyofikiri hadi kutenda.Sisi ni watumwa.Tumetengenezewa maisha fake na system fake zinazotufanya tuendelee kuwa watumwa.


Watetutemngenezea siasa,wametutengenezea mtindo wa maisha ambao ndani yake tunajitesa sana na kuhangaika na mambo yasiyokuwa na maana na kutufanya tuone maisha haya ni kitu cha maana sana wakati kuna mengi makubwa zaidi ya hayo hili nitalizungumza kwa kina siku nyingine,lakini kuanzia kufikiri,kuvaa,kutenda na yote sisi ni watumwa,tunaendeshwa kwa remote kutoka mahali fulani....

Haya yote,uwepo wa viumbe ambao wana uwezo zaidi kuliko binadamu na yote ni kuonesha kuwa binadamu yupo hatarini lakini hawezi kuwa hatarini kama hakuna uwezo wa kutoka kwenye hatari hiyo,je unasdhani ni ipi?

Tukutane wakati mwingine wakuu....
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment