BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA AFYA ATAKA WAGANGA WA TIBA ASILI WASIWEKEWE VIKWAZO NA WAGANGA WA HOSPITALI ZA MIKOA


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kutowawekea vikwazo wataalamu wa tiba asili na mbadala ili waweze kujisajili na kutambulika kisheria.

Mwalimu ameyasama hayo jana wakati akizindua Mpango Mkakati wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala utakaoanza kutumika mwaka 2017 hadi mwaka 2022.

Amesema si lengo la Serikali kukandamiza au kuzuia tiba asilia bali inataka kuhakikisha dawa zinazotumika ni salama kwa afya za watumiaji.

“Ili kujua kama dawa ni salama lazima wajisajili, dawa zao ziangaliwe na inapothibitika kuwa ni salama basi zitumike, tusiwawakee vikwazo, ni wajibu wetu kuwawekea mazingira wezeshi kufikia hatua hiyo,” amesema.

Amesema zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia tiba mbadala na asilia hivyo ni muhimu kuwepo uangalizi wa kutosha kuhakikisha dawa hizo hazileti madhara kwenye jamii.

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Edmund Kayombo amesema watalaamu 16,200 pekee ndio wamesajiliwa kisheria kutoa tiba hizo. 


“Tunawahamasisha waje kujisajili, wapo wanaojitokeza ila wengi wao wanakwepa kwasababu hawataki kuonyesha miti wanayotumia,”amesema.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: