BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BOMOABOMA YAWAONDOA PORINI WATU 1,000 KWA ULAZIMA GEITA

Geita. Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Geita kwa kushirikiana na wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wameanza operesheni ya kuwaondoa kwenye maeneo ya hifadhi za misitu wananchi waliovamia maeneo hatari ya mlima wa Geita.

Wananchi zaidi ya 1,000 wameathirika na bomoabomoa hiyo iliyoanza leo Ijumaa saa tatu asubuhi.

Akizungua katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema serikali ya wilaya imetimiza agizo la kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa cha Oktoba mwaka jana kilichotangaza wananchi hao wahamishwe katika maeneo hayo.

Wakizungumza na waandishi baadhi ya wananchi balozi wa eneo hilo Cleofas Vitalis amesema wanaishi katika eneo hilo toka mwaka 2002 na walinunua maeneo kutoka kwenye uongozi wa Mtaa wa Mkoani ambao zamani kilikua Kitongoji cha Mkoani.

Amesema wamepewa taarifa ya kutakiwa kuhama maeneo hayo miezi miwili iliyopita lakini hawakuhama wakiamini Serikali itawahurumia kwa kuwa hawana pa kwenda na tayari wana watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Mkoani. 


Wanafunzi zaidi ya 100 wanaosoma Shule ya Msingi Mkoani wameathiriwa na bomoabomoa hiyo.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: