BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMANDA WA POLISI ARUSHA AWATAKA WAZAZI KUENDELEA KUWAKUZA WATOTO WAO KIMAADILI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu katika sherehe ya Mahafali ya darasa la Saba katika shule ya Msingi Nalopa .
 
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.
Wito umetolewa kwa wazazi, na kuelezwa kwamba mbali na kujitahidi kuwasomesha watoto wao katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwapatia elimu bora wametakiwa pia kuzingatia kuwapa makuzi mema ili uhalisia wao kimuonekano uendane na elimu wanayoipata.

Hayo yameelezwa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Omari Mkumbo wakati wa sherehe ya mahafali ya wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Msingi Nalopa iliyopo jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali hayo alisema kwamba, wanafunzi hao kwa sasa wanakwenda katika hatua nyingine ya kimasomo lakini pia umri wao unaongezeka na kukumbana na changamoto mbalimbali, hivyo wazazi wanatakiwa waendelee kuwakuza kimaadili ili elimu yao iwe na manufaa kwao na kwa jamii.

Alisema elimu wanayoipata ikiendana na maadili itawasaidia kuepuka kujiingiza katika vitendo vya uhalifu kama vile matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine wowote na hatimaye kuonekana kuwa wa thamani machoni mwa watu.

Kamanda Mkumbo aliwataka wanafunzi hao kuongeza bidii katika masomo yao hasa ya Sayansi ili idadi ya wataalamu wengi katika kada mbalimbali iongezeke hasa katika huu ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia ambao ushindani wa soko la ajira umekuwa mkubwa.

Akimkaribisha mgeni rasmi kuwatunuku vyetu wahitimu hao ambao walifanya vizuri kimasomo, kinidhamu, uongozi, kimichezo na kujituma, Mlezi wa shule hiyo Balozi Mstaafu Bw. Daniel Ole Njoolay alitumia nafasi hiyo kumpongeza Kamanda huyo kwa kuzidi kuimarisha hali ya usalama katika mkoa wa Arusha pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo.

Awali akizungumza katika Mahafali hayo Meneja wa shule hiyo yenye wanafunzi 461 Bw. Edward Njoolay alisema kwamba, awali akisoma wasifu wa shule hiyo alisema kwamba mwaka 1999 ilikuwa kama “Day Care” lakini ushawishi wa wazazi uliwawezesha kufanikiwa kufikia hatua kubwa kimiundo mbinu na kitaaluma.

Shule hiyo imefanikiwa kutoa wahitimu wa darasa la saba mara nane ukiondoa wahitimu wa jana na wote walifanikiwa kufaulu na kuendelea na masomo ya Sekondari ambapo mwaka 2016 ilishika nafasi ya saba katika shule bora za Halmashauri ya jiji la Arusha zilizofanya mtihani wa darasa la saba.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: