BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM INA DHAMBI INAYOKARIBIA MAUTI


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewafahamisha amesema kitu cha msingi ambacho wananchi wanatakiwa wajue ni kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefika mwisho na kusisitiza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na Chama hicho kina dhambi iliyokaribia mauti.

Kauli hiyo ameitoa jana Novemba 19,2017 katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu mkoani Mwanza ambako Mbowe alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017.

“Tundu Lissu yuko hospitali ana uguza majeraha ya risasi si kwa sababu alifumaniwa, si kwa sababu ni mwizi ni kwa sababu ya kupigani haki zenu, dhambi kubwa kuliko dhambi zote duniani ni uoga na sasa kitu cha msingi sana mjue tu kwamba CCM imefika mwisho".


Alisema Lema Na kuongeza "Mmesikia Zimbabwe waliompindua Rais Mugabe sio Wapinzani aliokuwa ana wapiga mabomu ni Wanajeshi aliwavalisha yeye vyeo, walewale machinga waliokuwa wanamshangilia Mugabe leo wameandamana kusema Mugabe toka.

Nitamshukuru Mungu sana siku nikiona hiyo siku inafika mahali hapa, mshahara wa dhambi ni mauti na dhambi ya CCM ni kubwa sana imekaribia kwenye mauti kwa sababu leo yupo Mwenyekiti wetu hapa na Katibu wetu Mkuu yuko mahali hapa na Lazaro Nyalandu yuko hapa,” alisema Lema.Nipashe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: