BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS MAGUFULI AKERWA NA UTENDAJI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUFUMBIA MACHO UVAA WA NUSU UTUPU

RAIS John Magufuli ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari vinavyotangaza muziki wakati wachezaji wakiwa wako nusu uchi.

Mbali na kuitaka Wizara na TCRA kuchukua hatua, Rais Magufuli pia aliitaka Jumuiya ya Wazazi kusimamia maadili ya Watanzania yaliyoanza kutoweka taratibu. Aliyasema hayo wakati akiwahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania alioufungua mjini Dodoma jana.

Rais Magufuli alisema kuwa yeye ni shabiki mzuri wa muziki, lakini cha kusikitisha kila anapofungua muziki, wanaoonekana kucheza wakiwa utupu ni wanawake na siyo wanaume. Alisema miziki ya aina hiyo inaharibu maadili ya watoto na siyo lazima iwe ndiyo miziki pekee ya kuchezwa.

Alisema umefika wakati kwa Watanzania bila kujali tofauti zao za kiitikadi, wayalinde maadili yao ya Kitanzania. Alisema maadili ya ku ‘copy’ na ku ‘paste’ yatalipeleka Taifa kubaya. “Kwa nini uwavulie watu wengine utupu wako?

Tena siyo kwa wakati muafaka? Niwaombe Jumuiya ya Wazazi, kila kinachotokea ambacho kinaenda tofauti na maadili ya Kitanzania, hata kama tunashindwa kuchukua hatua, basi tupige kelele; kelele zetu watu watazisikia na Mungu atazisikia,”alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, enzi za akina Mama Maria Nyerere na Fatma Karume mambo hayakuwa hivi kama leo na kukishangaa kizazi cha sasa kimekumbwa na mdudu gani. Alisema imekuwa vigumu kwa familia kukaa pamoja na kuangalia vipindi vya muziki kwenye televisheni kwa kuwa mambo yanayofanyika hapo ni aibu.

Alisema Jumuiya ya Wazazi ina wajibu mkubwa wa kukemea uovu huo unaovunja tabia njema za Watanzaia. Aidha, alivishangaa vyombo na wizara vinavyohusika kusimamia maadili nchini kukaa kimya wakati mambo hayo yakiendelea kuharibu maadili ya Watanzania.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria Mkutano huo wa Jumuiya ya Wazazi ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wastaafu wa Chama na Serikali, viongozi wa upinzani pamoja na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: