BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROF MUZALE ATAJA CHANGAMOTO NA VIKWAZO KWA VIZIWI TANZANIA


Mtafiti wa Isimu, Lugha ya alama Tanzania na Masuala ya Viziwi, Profesa Henry Muzale (katikati), Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita), Nidrosy Mlawa kulia na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sosiologia na Anthopolojia, Edidiu Kamanyi wakifurahia jambo wakati wa mafunzo hayo. Picha na Juma Mtanda.

Juma Mtanda, Morogoro.

Mtafiti wa Isimu, lugha ya alama Tanzania na Masuala ya Viziwi, Profesa Henry Muzale ametaja changamoto na vikwazo vinavyowakabilia viziri katika jamii huku akieleza kuwa vimekuwa vikiwaathiri katika maisha yao ya kila siku huku akiitaka jamii kuwa na jukumu la kutafakari na kusaka namna ya kuisaidia na kuzitatua.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa asasi katika masuala ya uwajibikaji wa jamii na michakato ya serikali za mitaa mjini hapa, Prof Muzale alieleza kuwa jamii na watalaamu wana kila sababu ya kupunguza ama kumaliza changamoto na vikwazo kwa viziwi.

Prof Muzale alieleza kuwa baadhi ya maisha ya viziwi imekuwa ikipata uziwi hadi siku ya mwisho ya uhai wake lakini njia ya kusaidia jamii hizo ni kuelimishana jinsi ya kuwasaidia kutatua changamoto na vikwazo ikiwemo kutetea haki za viziwi na watu wenye ulemavu na watoto viziwi kujengewa mwanzo mzuri wa mawasiliano.

“Sote tunafahamu kuwa lugha ni chombo kikuu kabisa cha mawasiliano baina ya wanadamu na lugha hufanikisha jambo lolote baina ya watu wawili au jamii kwa ujumla katika nja zote za maisha na bila lugha hakuna maendeleo, lakini jamii ya viziwi wamekuwa wakiminywa na lugha wanayoimudu zaidi na hilo ni kama kuinyanyasa jamii hiyo ya viziwi.alieleza Prof Muzale.

Prof Muzale alieleza kuwa changamoto za viziwi katika jamii ni pamoja na hukosa ujumbe na taarifa yanayoongelewa katika makundi mbalimbali lakini kuna njia za kupunguza baadhi ya changamoto kwao.

“Ili kupunguza baadhi ya changamoto kwa watoto viziwi, kwanza wazazi kuwapeleka shule maalumu ili kujifunza lugha ya alama na jamii ina jukumu la kuhamasisha mabadiliko ya kimtazamo nan kuondoa fikra potofu dhidi ya viziwi kuwa hakuna jambo wanaloweza.”alieleza Prof Muzale.

Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita), Nidrosy Mlawa alisema kuwa changamoto kubwa ni mawasiliano ndio inayowasababisha watoto viziwi kushindwa mambo mbalimbali wakianzia watoto hadi watu wazima.

Mlawa alisema kuwa mtoto kiziwi hukosa mawasiliano ngazi ya jamii na hiyo ndio humjenga mtoto na lugha hizo ni lazima ianzie nyumbani ili anapofika shuleni iwe rahisi kuanza na lugha lakini imekuwa tofauti kwa wazazi wengi kusababisha viziwi kukumbwa na vikwazo vikbwa kwao.

“Mtoto anapofika shuleni anakuwa hana lugha na hilo ni tatizo kwake lakini kama wazazi watamjenga mtoto kwa lugha ya alama inampunguzia vikwazo lakini serikali kama itatenga fungu la kujengewa uwezo kwa wazazi wenye watoto viziwi pamoja na walimu wa elimu maalumu kujengewa uwezo kwa lugha ya alama.”alisema Mlawa.

Mratibu wa Mradi katika mafunzo hayo, Lupi Maswanya alieleza kuwa mradi huo utalenga mikoa ya mitatu ikiwemo mkoa wa Mtwara, Tanga na Dodoma kwa kutoa mafunzo ya namna ya ushiriki mkubwa ni msingi wa kujenga uwezo wa asasi katika masuala ya uwajibikaji wa jamii na michakato ya serikali za mitaa.

Lupi alieleza kuwa tunaoma serikali yenyewe ibadilike kwanza na serikali mambo ya viziwi bado haijapokea viziru na viziwi wenyewe tayari imeanza kuangalia walemavu ngazi ya vijiji.


Mafunzo hayo yamelenga mafunzo ya namna ya kuimarisha utendaji na ufanisi katika utekelezaji wa mipango mikakati na kuangalia changamoto zitokanazo na migongano kati ya bodi za utekelezaji na watendaji wa katiba, dhana ya kuwa na utume wa shirika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: