BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UTEKAJI, KUPOTEA KWA WATU, MASHAMBULIZI YA SILAHA KWA VIONGOZI WA KISIASA NI TISHIO LA KUTOWEKA KWA AMANI YA TANZANIA

Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.

Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji

yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.

"Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na

kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na

ubabe, vurugu, hila, na vitisho", imesomeka sehemu ya waraka huo

Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.

Ujumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki

"Shughuli za kisiasa kama vile maandamano, mikutano ya hadhara, ambayo ni haki ya kila raia, vinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola", inasomeka sehemu ya waraka huo wa Maaskofu wa kanisa Katoliki

Maaskofu wa Katoliki waligusia pia kuminywa kwa uhuru wa kutoa na kupokea habari huku wakitaja baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa au kusimamishwa kwa muda.

Walionya kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.

Maaskofu wa KKKT wameasa kwamba roho iliyokuwemo kwa waasisi wa taifa na hata kusaidia kupata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu, inapaswa kuendelea wakati wote

"Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru na Umoja ndizo ngao zetu

zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50", wamesema maaskofu wa KKKT.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: