BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAANDISHI WAPIGWA NA KUJERUHIWA WAKATI WA TUKIO LA KUZUILIWA KWA ALIYEMWAPISHA RAILA ODINGA KUWA RAIS KENYA

Odinga alijaribu kumsaidia Miguna kuondoka uwanja wa ndege bila mafanikio

Nairobi. Wakili wa upinzani aliyeidhinisha kiapo cha Raila Odinga alipokuwa anajiapisha kuwa 'Rais wa Wananchi' mwezi Januari bado amekwama katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya.

Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada yake kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Wakili huyo alisisitiza kwamba ni raia wa Kenya na hafai kuzuiwa kurejea.

Taarifa zinasema Miguna, ambaye pasipoti yake ya Kenya ilitwaliwa na polisi kabla ya kuondolewa kwake Kenya mwezi jana, alikuwa ametakiwa kuwasilisha ombi la kupata visa ya kukaa Kenya kwa miezi sita kwa kutumia pasipoti hiyo yake ya Canada.

Alikataa jaribio hilo na badala yake kutoa kitambulisho chake cha taifa kuonesha kwamba yeye ni Mkenya na kutaka aruhusiwe kuingia.

Miguna, aliyekuwa amewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa nane adhuhuri, alikesha kwenye uwanja huo.

Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

Wakili wa upinzani, James Orengo seneta ambaye majuzi alichaguliwa kuwa kiongozi wa upinzani Bunge la Seneti, ameambia Reuters kwamba maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ndio waliojaribu kumlazimisha Miguna kupanda ndege hiyo iliyokuwa inaondoka.

Lakini wakili huyo alikataa kuingia ndani ya ndege hiyo na mtafaruku ukazuka.

Video iliyopeperushwa moja kwa moja na runinga ya kibinafsi ya Citizen ilimuonesha Miguna akiwa kwenye lango la ndege akiwaambia wahudumu: "Siendi popote, hamuwezi kuniondoa kutoka kwa nchi yangu kwa nguvu."

Orengo ameambia Reuters kwamba maafisa hao wa polisi baadaye walimuondoa mwanasiasa huyo kutoka kwenye ndege hiyo na kumzuilia kwa muda katika afisi za uhamiaji katika uwanja huo wa JKIA.

Baadaye asubuhi, walimhamishia kituo cha polisi cha uwanja huo na kuendelea kumzuilia.

Odinga alikuwa amefika uwanjani humo Jumatatu usiku kujaribu kutatua mzozo huo.

Kwa mujibu wa Orengo, Odinga alikuwa ametoa wito kwa serikali kumrejeshea Miguna pasipoti yake ya Kenya.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uhamiaji mapema Jumanne ilisema Miguna alianza "kuzua fujo na kulalamika" uwanja wa ndege na kwamba alikuwa anataka kuruhusiwa kuingia Kenya bila kuidhinishwa na maafisa wa uhamiaji.

Wizara hiyo imesema inafanikisha utaratibu wa kumuwezesha Miguna kuwasilisha tena ombi la kuwa raia wa Kenya.

Taarifa ya wizara hiyo ilisema fomu za kuwasilisha maombi hayo zimetumwa uwanja wa Ndege.

Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji, Joseph Munywoki kwenye taarifa alisema: "Badala ya kuonesha hati za kusafiria alizotumia kwenda Canada, Miguna alianza kuzua fujo na kulalamika akisema kwamba yeye ni Mkenya na anafaa kuruhusiwa kuingia Kenya bila kupitia kwa meza ya idara ya uhamiaji kama inavyotakiwa kwa abiria wote wanaowasili bila kujali uraia wao."

"Hatujamzuia kuingia Kenya, tunamtaka tu afuate utaratibu kama watu wengine wote," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani

Mwenda Njoka aliambia Reuters kwa njia ya simu.

Idara ya uhamiaji ya Kenya imekariri kuwa Miguna alipoteza uraia wa Kenya mwaka 1988 alipopewa uraia wa Canada wakati alipokuwa ni kinyume cha sheria kuwa na uraia wa nchi mbili nchini Kenya.

Kuzuiliwa kwa Miguna kumejadiliwa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii Kenya, baadhi wakiunga mkono hatua hiyo lakini wengine wakiwashutumu maafisa wa uwanja wa ndege na serikali.


Kukamatwa kwa Miguna mara ya kwanza
Miguna alikamatwa na polisi kwa mchango wake katika kuapishwa kwa Odinga kuwa "rais wa wananchi", hafla iliyofanyika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi mnamo 30 Januari.

Miguna, ambaye pia ni wakili, ndiye aliyetia saini hati ya kiapo ya Odinga.

Serikali ilikuwa imeeleza hatua hiyo ya kiongozi huyo wa upinzani kuwa uhaini wa hali ya juu.

Odinga anadai kwamba alimshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa 8 Agosti ambao matokeo yake yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kutokea kwa kasoro nyingi.

Mahakama iliamuru uchaguzi mpya ufanyike lakini Odinga akasusia uchaguzi huo mnamo 26 Oktoba.

Polisi nchini Kenya wamejipata tena wakishutumiwa kwa kuwapiga na kuwajeruhi waandishi wa habari wakiwa kazini.

Polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia waliwashambulia waandishi wa habari wa magazeti na televisheni na wapiga picha Jumatatu usiku walipokuwa wakifuatilia taarifa kuhusu kurejea Kenya kwa Miguna.

Maafisa hao, ambao hawakufurahishwa na ufuatiliaji wa vyombo vya habari wa taarifa ya kurejea kwa mwanasiasa huyo waligeuza hasira zao kwa waandishi wa habari na kuwaumiza baadhi yao.

Mpigapicha wa televisheni ya NTV aliachwa akiwa na majeraha yaliyokuwa yanavuja damu huku kamera na vifaa vyake vya matangazo ya moja kwa moja vikiharibiwa na maafisa hao wa usalama.

Alikuwa akitangaza tukio hilo moja kwa moja alipovamiwa na polisi

Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Citizen Steven Letoo pia alijeruhiwa na vifaa vyake vikachukuliwa.

Naye mwanahabari wa KTN News Sophia Wanuna alizabwa kofi na mmoja wa maafisa hao.

Miguna, ambaye alishuhudia shambulio hilo alilalaani kitendo hicho cha polisi.

"Wamefukuza vyombo vya habari kama sungura," alimwambia rubani wa ndege ya Emirates huku akikataa kuondoka na ndege yake.

"Wanawafukuza wanahabari."
Viongozi wamelaani leo shambulio hilo, huku mbunge wa Rarieda
Otiende Amolo akielezea kitendo hicho kama "cha kusikitisha".

Amevitolea wito vyombo vya habari kuchukua hatua za kisheria dhidi ya maafisa husika na makamanda wao.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: