BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KIFO CHA VIDEO QWEEN AGNES GERALD 'MASOGANGE' HIKI NDICHO KILICHOIBUA


Dar es Salaam. Msanii anayepamba video za muziki (video queen), Agnes Gerald ‘Masogange’ amefariki dunia leo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mwanasheria wake, Reuben Simwanza, alipozungumza na Mwananchi leo Aprili 20.

Simwanza amesema taarifa za kifo chake amezipata kupitia dada yake, saa chache zilizopita.

Kwa maelezo ya Simwanza, dada wa Masogange, Emma Gerald, ndiye aliyetoa taarifa hizo baada tu ya kutoka kumuona alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo ambaye amedai yeye si msemaji zaidi, kuhusu nini chanzo cha kifo chake, alidai mara ya mwisho waliwasiliana naye siku mbili zilizopita kwa ujumbe wa simu ya mkononi.

“Unajua kuumwa kweli alikuwa anaumwa, kipindi cha kesi yake magonjwa ya hapa na pale ikiwamo presha, si unajua tena mambo ya kesi hayana mwenyewe, lakini baada ya kwisha tulikuwa tunataniana kwamba sasa nina imani utakuwa powa kwani kila kitu kipo sawa,”amesema Simwanza.

Hata hivyo amesema yupo njiani kuelekea hospitali kwa kuwa hakuweza kupata maelezo zaidi kutoka kwa dada yake huyo ambaye amemsikia akiwa analia tu.

Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017.
Wasanii mbalimbali nchini wameonyesha masikitiko kupitia mitandao yao ya kijamii, baada ya kupata taarifa za kifo cha msanii mwenzao, anayepamba video za muziki, (Video Queen) Agnes Gerald maarufu Masogange.

Wakili wake, Reuben Simwanza amezungumza na MCL Digital na kuthibitisha kuwa Masogange amefariki leo.

Aslay Isihaka ameweka picha ya Masongange na kuandika, “Dah mbele yako nyuma yetu sister, safari yetu moja innalillah wainnailah raajiun,”

Huku Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnum’ akiweka picha ya mishumaa na maneno, “Rest in paradise Agnes.”

Rajab Kahali ‘Harmonize’ ameweka picha ya Masongange na kusema, “God’s plan R.I.P. Aggy.

Naye Steven Mengere 'Steve Nyerere’ ameweka picha tatu tofauti za Masogange na kuzungumzia kifo hicho akianza kwa kusema;

“Nimepokea taarifa ya kifo chako kwa mshtuko mkubwa sana. Masogange amka mama Masogange. Staki kuamini.”

Mcheza filamu, Wema Sepetu ameweka picha ya Masongange ikiambatana na maneno, “Innah lillah wa innah illah rajiun... Dah...!.Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: