BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIONGOZI WA CHADEMA NA WENGINE TISA WAMAKATWA NA JESHI LA POLISI TUHUMA ZA MAANDAMANO DAR


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limewakamata watu tisa kwa tuhuma za kufanya maandamano.

Akizungumza na MCL Digital leo Aprili 26, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Mtaa wa Samora, Posta katikati ya mji.

"Tumewakamata watuhumiwa tisa akiwamo, mwanafunzi wa Chuo cha Kilimanjaro kilichopo Mwenge akiwa na bango linalohamasisha maandamano," amesema Mambosasa na kuongeza:

“Tunaendelea kumhoji na wenzake wanane, tutakapokamilisha mahojiano hatua zaidi zitafuata.” Kuhusu hali ya usalama Kamanda Mambosasa amesema jeshi limejipanga kuimarisha ulinzi usiku na mchana hakuna mtu yeyote atakayevunja sheria.

Kiongozi wa Chadema akamatwa.
 

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limedhibitisha kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake la Chadema, Elizabeth Mambosho (Pichani).

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Aprili 26 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro amesema wamemkamata na kumuhoji kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao.

"Ni kweli tulimkamata jana usiku na kumuhoji kwa kosa la kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao na tumemwachia kwa dhamana," amesema Muliro.

Amesema kuwa wanaendelea na upelelezi utakapokamilika akibainika anakosa watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma.

Kuhusu polisi kuzagaa mtaani amesema Jeshi la Polisi lina utaratibu wa kuimarisha ulinzi kila kunapokuwa na sikukuu za kidini na zile za kiserikali.

"Ni kweli polisi wetu wako kwenye doria maeneo yote ni utaratibu wetu kila kunapokuwa na sikukuu za kidini na zile za kiserikali hivyo watu wasiwe na wasiwasi waendelee na shughuli zao kama kawaida," amesema Muliro.

Amewataka wakazi wote kuachana na uvunjifu wa sheria hasa kwa njia ya mtandao kwani jeshi liko imara kupambana na wahalifu watakaojaribu kuvunja sheria.Chanzo/Mwananchi
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: