
Mshambuliaji wa klabu ya Mawenzi Market FC ya Morogoro, Hassan Mkota kulia akichuana na mlinzi wa KMC, Salum Mlima wakati wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2016/2017 uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro na Mawenzi kutandikwa bao 2-1. Picha na Juma Mtanda
Na Juma Mtanda, Morogoro.
Klabu ya Mawenzi SC iliyopo ligi daraja la kwanza imepewa mchongo wa kupata fedha ili kuondokana na tabia ya kutembeza bakuli wakati wa michezo ya ligi hiyo katika msimu wa mwaka 2018/2019 mkoani Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Katibu Mtendaji wa soka wilaya ya Morogoro (MMFA), Kafale Maharagande amesema kuwa ili Mawenzi SC iepukanane na kutembeza makuli wakati wa ligi hiyo ikiendelea, ianze kwanza kuingiza wanachama wapya wataoweza kuichangia timu wakati ina uhaba wa fedha.
Maragande amesema kuwa vibabu vingi vya Tanzania vimekuwa vikiyumba kwenye ushiriki wa ligi mbalimbali kutokana na kuwa na wanachama wachache na kuwa jambo hilo linaikwamisha timu pindi inahitaji fedha za kutatulia jambo lililopo mbele yao.
“Vilabu vingi vinavyoshiriki ligi daraja la tatu hadi ligi kuu Tanzania bara havina wafadhili ambao wanasaidia mambo mengi kwenye timu lakini mimi naona njia ya kuepukana na suala la kutembeza makubali si jambo zuri wakati timu tayari ipo kwenye mashindano.”alisema Maharagande.
Maharagande amesema kuwa kwanza timu zifanye ushawishi wa kuingiza wanachama wapya ili klabu iwe na wanachama wengi na hao wanachama wanaweza kuichangia timu wakati wa matatizo bila kuiathiri kipindi chote cha mashindano au ligi.
Kwa upande wa Katibu mkuu Mtendaji wa klabu ya Mawenzi SC, Juma Kilangilo amesema kuwa klabu hiyo kwa sasa tayari ina wanachama 70.
Kilangilo amesema kuwa klabu inatarajia kufanya uchanguzi mkuu wa kuchagua viongozi baada ya waliopo kumaliza muda wao.
“Kamati ya uchanguzi tayari imeundwa chini ya Mwenyekiti wake Kafale Maharagande na ametoa ushauri wa sisi viongozi tuongeze wanachama ili waweze kuisaidia timu pindi inapokwama na hilo ndilo tunalitekeleza.”amesema Kilongilo.
Klabu ya Mawenzi SC iliponea tundu la sindano kushuka daraja msimu huo wa mwaka 2016/2017 kutokana na kuyumba katika ligi daraja la kwanza huku sababu kubwa ikiwa mfadhili wa klabu hiyo kujiondoa katikati ya ligi kutokana na mikwaruzano ya kimaslahi.

0 comments:
Post a Comment