BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC HAINA PRESHA NA MTIBWA SUGAR


Na Juma Mtanda, Morogoro.
Simba Sc imesema itashusha kikosi kamili dhidi ya Mtibwa Sugar huku ikitegemea zaidi nguvu za mungu ili kuondoka na alama tatu muhimu na kuendelea kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara 2017/2018 katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali unaopigwa (leo) kwenye uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza na MTANDA BLOG uwanja wa jamhuri Morogoro jana, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kuwa benchi la ufundi halina presha na mchezo huo licha kuwa wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Mtibwa Sugar.

Djuma amesema kuwa Mtibwa Sugar si timu ya kubeza na imeingia nusu fainali ya FC kwa kuilaza Singida United ao 3-0 nyumbani kwao lakini benchi lao la ufundi haliwatishi na ushindi huo na wamejiandaa vyema kuhakikisha wanacheza kwenye kiwango bora na kuhakikisha wanavuna na alama tatu muhimu licha ya kuwaheshimu.

“Mtibwa Sugar si timu ya kubeba na imeingia nusu fainali ya kombe la FA kwa kuiondosha Singida United, hivyo hilo halitupi presha kwetu kwani tumejiandaa na kuandaa kikosi imara cha kukabiliana nao kwenye uwanja wao wa nyumbani ili tupate ushindi na kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi kuu.”alisema Djuma.

Aliongeza kwa kusema kuwa Simba wanalazimika kuitetea nafasi ya kwanza kwa udi na uvumba lakini endapo watateleza watakuwa wamepata shida lakini hilo si tarajio lao japo hali ya mchezo wa soko una matokeo matatu.

Djuma alisema kuwa wataendelea kupambana kuhakikisha wanavuna pointi tatu kila mchezo uliopo mbele yao huku kila mchezaji akielewa majukumu yake ndani ya uwanja na kuomba mashabiki kuwaombea dua njema. 


“Wachezaji waliokuwa na matatizo wameanza mazoezi na wenzao na jana (juzi) tumefanya mazoezi uwanja wa jamhuri Morogoro na baada ya kupata pointi tatu dhidi ya Njombe Mji, benchi la ufundi na wachezaji wameelekeza akili kwenye mchezo wetu na Mtibwa Sugar.”alisema Djuma.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: