BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SHULE YA MSINGI YAHITAJI SH 13.6MILIONI ILI KUMALIZA UKARABATI WA MADARASA WA VYUMBA TISA.

JUMLA ya shilingi 13.6 Milioni zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa vyumba tisa vya madarasa katika shule ya msingi Misufini A kata ya Mafiga Manispaa ya Morogoro vilivyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kusababisha wanafunzi kulundikana katika madarasa tisa ambayo ni salama ili kuendelea na masomo hali iliyodumu kwa miezi 11 sasa.


Akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa saruji mifuko 70 kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii (PPF) Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Misufini A, Jane Mlangwa alisema kiasi cha sh 13,673,000 Milioni zinahitaji ili kuweza kumalizia kazi ya ukarabati wa vyumba tisa vilivyoezuliwa na upepo mkali ambao uliambatana na mvua iliyonyesha february 5 mwaka huu na kusababisha hasara hiyo.


Mlangwa alisema kuwa baada ya kupata hasara hiyo wafadhili mbalimbali mkoani hapa walijitokeza kusaidia vifaa mbalimbali kama fedha,bati, mbao na saruji kwa lengo la kufanya ukarabati katika vyumba hivyo tisa vya madarasa ili wanafunzi waweze kupata maeneo ya kusomea ambapo kwasasa wanafunzi hao wanalazimika kutumia madarasa kwa zamu katika kusoma.


Alivitaja vyumba vya madarasa ambavyo vimeathiriwa na upepo huo kuwa ni pamoja na darasa la awali, darasa la kwanza A, tatu A na B, nne A na 5 na darasa la sita A na B pamoja na sehemu ya kuhifadhia vifaa.


Aidha Mlangwa aliwataja wafadhili walioisadia shule hiyo msaada wa vifaa na fedha taslimu kuwa ni pamoja na benki ya NMB mbayo imetoa mbao zenye thamani ya sh 6,000,000, PPF ambayo imetoa mifuko ya saruji 70 ikiwa na thamani ya sh 1,080,000, Kiwanda cha Tumbaku (TTPL) kimetoa vitabu vya kiada na ziada katika darasa la tano na sita vyote vikiwa na thamani ya sh 6,372,000 milioni.


Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha, Msatafa Mkulo sh 500,000, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro sh 7,475,000 milioni, Wazazi wa shule hiyo sh 400,000 na Baraza la Maendeleo ya kata Mafiga sh 500,000. Ambazo zote hizo zikiwa na jumla ya 22,327,000 milioni.


Pia Mlangwa alisema kupatikana kwa misaada hiyo pia imesaidia kupunguza baadhi ya matatizo ikiwemo tatizo la vitabu kwa wanafunzi wa darasa la tano na sita na kuwa tatizo hilo limeisha na kuyataja matatizo mengine ambayo bado yanahitaji msaada wa wafadhili.


Amebainisha tatizo hilo ni pamoja na madawati kwa wanafunzi wa shule ya awali,darasa la kwanza A, darasa la pili A, darasa la tatu A na B na darasa la nne pamoja na kupata saruji kwa ajili ya sakafu katika vyumba vya madarasa hayo yote.


Naye Mwasibu Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kanda ya Mashariki na Kati (PPF) Philimon Kamanga akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Kanda hiyo, Jarome Ng’itu alisema mfuko huo umekuwa ukitoa msaada kwa jamii katika majanga mbalimbali kulingana na uzito wa tatizo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: