BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ANADAI JESHI LA POLISI ARUSHA LILIKUWA SAHIHI KUZUIA MAANDAMANO YA CHAMDEMA.


MWANASHERIA WA JINSIA NA WATOTO, DAVID MSUYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MJINI MOROGORO.

IMEDAI kuwa jeshi la polisi katika mkoa wa Arusha lilikuwa lipo sahihi katika kuzuia maandamano ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuwa vurugu zilizotokea katika mji huo zimechangiwa na taarifa zisizo rasmi za kupewa kibali chama hicho cha kufanya maandamano ya amani na kuwa taarifa hizo hazikuwa sahihi huku watu wawili wakiripotiwa kufariki dunia katika vurugu hizo zilizotokea januari 5 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Jinsia na Watoto, David Msuya ambaye ni mkazi wa jiji la Arusha wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Morogoro ambapo alisema kuwa jeshi hilo lilikuwa lipo sahihi kuzuia maandamano hayo kwa madai kuwa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) hawakuweza kupata kibali cha kufanya maandamano hayo ya amani kutoka kwa jeshi la polisi mkoani humo.

Msuya alisema kuwa jeshi la polisi linalo mamlaka ya kutoa kibali au kuzuia kutoa kibali kwa kuangalia aina ya maandamano ambayo waombaji watafanya yatakuwa na athali gani kwa wananchi na yatapokelewa na kiongozi gani na kama kutakuwa na kiongozi ambaye jeshi hilo linamtilia mashaka ya uvunjifu wa amani na kuchochea vurugu basi jeshi hilo haliwezi kutoa kibali.

Msuya alisema kuwa kufanya maandamano bila ya kuwa na kibali ni kukaidi amri ya jeshi la polisi na unapokaidi na kufanya maandamano unakuwa unazalisha vurugu na badala yake jeshi litafuata taratibu za kisheria.

Kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya muungano wa Tanzania sura ya 3 hadi 41kufanya vurugu au uchochezi ni sawa kosa la shitaka la mauaji na kuwa jeshi la polisi hatakuwa na kosa kuzuia maandamani hayo ya namna hiyo. Alisema Msuya.

Aidha Msuya alisema kwa mujibu wa taratibu za jeshi la polisi ambalo limeundwa kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haliwezi kutoa kibali na baadaye likabadilisha maamuzi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyem na taratibu za sheria na kama kutakuwa na askari ambaye atakeuka taratibu hizo atakuwa ameenda kinyeme na taratibu za kisheria na anapaswa kumwajibishwa kisheria.

“polisi inapozuia maandamano basi kuna kitu kimeona mbele yake kitatokea ikiwemo ya uvunjifu wa amani ikiwemo mali za wananchi wake kwa eneo husika na hali hiyo ikitokea jeshi la polisi itachukua jukumu la kutawanya maandamano ili kuzia uvunjivu wa amani” alisema Msuya.

Msuya alisema kuwa pakuwa kazi ya jeshi la polisi ni kulinda haki ya kila raia na mali zake na kudai kuwa jeshi linaendeshwa kwa sheria na amri kwa hivyo wanapokukamata mtuhumiwa kwenye tukio lolote litatumia uwezo wa nguvu za kisheria ili kuweza kukufikisha kituoni kwa ajili ya mahojiano ya tukio husika. Alisema Msuya.

Pia Msuya ametoa ushauri kwa waziri wa mambo ya ndani Shamsi Vuai Nahodha kuwa katika suala zima la la ulinzi wanchi na mipaka yake halina siasa na kinachotumika zaidi ni amri na kueleza hali hiyo ndiyo iliyotokea kwenye Jiji la Arusha.

Ni aibu kubwa kwa Tanzania zima kutokana na tukio lililojitokeza katika mji wa Arusha kwani baadhi ya nchi nyingi za afrika zimekuwa zikipata ushauri wa kisiasa na mambo mbalimbali.

Katika vurugu zilizotokea Januari 5 mwaka huu watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha kwa mujibu wa kamanda wa mkoa huo Thobias Andengenye wakati jeshi la polisi mkoa huo likitawa waandamanaji wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema huku watu kadhaa wakijeruhiwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

Anonymous said...

Asante Mwanaglobu

Naomaba nichaingie mambo muhimu kwa huyo mwanaharakati wemu kibali cha kufanya mikutano ya kisiasa polisi hawana mamlaka ya kutoa kibali hiyo ni kazi ya ofisi husika.

Pia polisi hawakupaswa kutumia nguvu zaidi katika kuzuia maandamano yale tunajua maji ya kuwasha yapo, mabomu ya machozi yapo ikishindikana virungu hutumika lakini sio kukurupuka na kutumia silaha za moto.

kitendo cha kutoa habari eti mwanasheria tena mwanaharakati wakati huohuo unakuwa umelalia upande mmoja tena haramu si sawa hutendi haki kwa wanaharakati.

Naamini macho yako na moyo wako hauoni wala hauhisi haki za binadamu kweli unaonesha jinsi ulivyosheheni mahaba na wakosaji amabo wako chini ya mwamvuli wa Serikali ambao ni ccm.

Natia shaka kuwa wewe hauwashi taa watu kuona kilichokuwepo ndani bali unazima taa watu wasione ndani hivyo si sawa.

Pia jaribu kutumia elimu uliokuwa nayo kuelimisha umma ukweli wa mambo sio kuwa bayasi.