BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHIALO KUFUNGA MASHINDANO YA LIGI DARAJA LA PILI NETIBOLI FEBRUARI 24.

KAMANDA wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro (SACP) Adolfina Chialo anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli wakati wa ufungaji michuano hiyo februari 24 katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mjumbe wa Kamati ya Utendaji katika chama cha Netiboli Tanzania Chaneta, Mwajuma Kisenga alisema kuwa mgeni rasmi wa kufunga mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa netiboli anatarajiwa kuwa Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro Sacp, Adolfina Chialo katika mchezo ambao utawakutanisha timu zinazomilikiwa na jeshi la polisi hapa nchini baina ya timu ya Polisi Arusha na timu ya Polisi Pwani ambao utachezwa majira ya saa 9 alasiri katika uwanja huo wa Jamhuri mjini hapa.


Kisenga alisema Kamanda Chialo ndiye aliyepitishwa na kamati ya mashindano hayo kuwa mgeni rasmi na anatarajia kuingia mapema katika uwanja huo hivyo na kuwaomba wakazi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake kufika katika uwanja wa Jamhuri kuangalia michezo ya ufungaji kwani kufanya hivyo itakuwa jambo la busara kwao hasa akinamama na wasichana wajitokeze kwa wingi ili kuweza kushuhudia wenzao wakicheza mchezo huo ambao utakuwa na ufundi wa hali ya juu katika kutoa pasi na kuonyesha uhodari wa kufunga mabao na hii inatokana na timu hizo kuwa na wachezaji wenye wengi wenye vipaji vya hali ya juu katika mchezo huo huo ambao utakuwa kufunga mashindano hayo.


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Chama cha Netiboli Tanzania Chaneta Mary Protasi alisema kuwa katika michezo iliyochezwa majira ya saa 10 jioni jana katika muendelezo wa mashindano hayo katika hatua hiyo ya robo fainali ligi hiyo ilishuhudia timu kutoka mikoa ya kanda ya kusini zikionyeshana kazi kwenye uwanja wa Jamhuri baada ya Kurugenzi Tandahimba ya Mtwara kukubali kipigo kutoka kwa ndugu zao wa mkoa wa Lindi timu ya Kurugenzi Ruanga kwa kufungwa bao 45-13.


Protasi alisema timu ya Kurugenzi Ruangwa ilionyesha dalili za ushindi mapema baada ya kuwadhibiti Tandahimba kila idara na kushinda kupenyeza mipira kwa wafungaji wao katika mchezo huo hasa katika kipindi cha kwanza baada ya kwenda mapumziko Ruangwa wakiongozajumla ya bao 21-5.


Mfungaji Khadija Othuman wa timu ya Ruangwa aliweza kutumia vema nafasi alizopata wakati alipokaribia langoni mwa wapinzani wao baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya bao 24 katika huo huku Naima Ramadhan akifunga bao 21 wakati wa wafungaji wa timu ya Tandahimba Nasra Selemani aliweza kufunga jumla ya bao 10 na wenzake Magedalena Luambano akichangia bao tatu katika timu yao na kufanya mchezo huo kumalizika kwa bao 45-13. alisema Protasi.


Pia Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ufundi katika chama cha Netiboli Chaneta alitaja matokeo ya michezo mingine iliyochezwa jioni hiyo ya februari 22 kuwa Hamambe ya mkoa wa Mbeya iliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 32-19 dhidi ya timu mwenyeji wa mashindano hayo Allianve One ya mkoani Morogoro nayo Tigo ya Dar es Salaam iliweza kupoteza mchezo wake kwa Polisi Pwani baada ya kukubali kutandikwa bao 42-15 wakati JKT Ruvu ilipokea kichapo kutoka kwa akinadada wa jeshi la Polisi Arusha cha bao 22-13.


Protasi alisema katika michezo mingene itayochezwa katika uwanja huo wa Jamhuri februari 24 itakuwa kati ya timu za Hamambe ya Mbeya ambayo itajitupa uwanjani kucheza na Tandahimba huku Alliance One ikionyeshana kazi na JKT Ruvu wakati Tigo ya Dar es Salaam nayo itapambana na Ruangwa michezo ambayo inatarajiwa kucheza mapeama kabla ya mchezo wa kufunga dimba ya mashindano hayo mjini hapa kati ya Polisi Arusha na Polisi Pwani.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: