NANE ZAFUZU ROBO FAINALI LGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI
MCHEZAJI WA HAMAMBE YA MBEYA DOTTO DOTTO AKITAFUTA MBINU YA KUMTOKA MCHEZAJI WA IMMAKULATA CHARLE WA POLISI PWANI WAKATI WA LIGI DARAJA LA PILI NGAZI YA TAIFA NETIBOLI UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO NA HAMAMBE ILISHINDA KWA BA0 31-16.
JUMLA ya timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika mashindano ya ligi daraja la pili ngazi ya taifa michezo itayochezwa februari 21 katika uwanja wa ndani wa Jamhuri yanayoendeelea mkoani Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika uwanja wa Jamhuri mara baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi kutoka chama cha mchezo huo taifa Mary Protasi alisema kuwa baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi jumla ya timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali michezo itayochezwa februari 21 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Protasi alitaja timu ambazo zimefuzu katika hatua hiyo kuwa ni Hamambe ya mkoani Mbeya ambayo imeongoza katika kundi A huku timu ya Polisi Pwani kishika nafasi ya pili wakati Ruangwa ikishika nafasi ya tatu na mwenye wa michuano hiyo Alliance One ikishika nafasi ya nne.
Katika kundi B Mwenyekiti huyo alizitaja timu ya Polisi Arusha kuwa ndiyo iliyongoza ikifuatiwa na JKT Ruvu ya mkoani Pwani huku timu ya Tigo ya Dar es Salaam ikiwa na nafasi ya tatu huku timu ya Kurugenzi Tandahimba ya mkoanbi Mtwara ikishika nafasi ya nne katika kundi hilo.
“timu nane zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali na tutatumia mfumo wa ligi na baada ya kumalizika kwa michezo yote tutampata mshindi wa kwanza na wane ambao watapanda hadi ligi daraja la kwanza lakini wakati huo huo itategemea na timu ambazo hazikushiriki ligi daraja la kwanza mwaka jana na kati ya timu hizo kama hatadhibitisha tutakuwa na uwezo wa kuzipatisha timu nyingine kucheza ligi daraja hilo, alisema Protasi.
Aidha Mwenyekiti huyo wa kamati ya Ufundi kutoka chama cha netiboli taifa alisema kuwa katika msimu wa mashindano ya ligi daraja la kwanza mwaka 2010/2011 zaidi ya timu nne hazikuweza kucheza ligi hiyo kutokana na matatizo mbalimbali ambapo mwaka huu itawalazimu chama chicho kuandikia barua ya kuthibitisha ushiriki wao mapema ili wasifuruge utaratibu wa kuwa na timu 18 katika ligi daraja la kwanza mara baada ya ligi daraja la pili kuisha.
“tayari tumewandikia barua timu zote ambazo hazikuweza kushiriki mashindano ya ligi daraja la kwanza kwa msimu wa 2010/2011 na sababu kubwa ya kufanya hivi ni kutaka tuzifuruge utaratibu uliopo kwa kuwa na timu 18 na timu ambayo itashindwa kuthibitisha kushiriki ligi daraja la kwanza msimu huu tutaangalia kati ya timu zilizofanya vizuri kuzipandisha hadi ligi daraja la kwanza”.alisema Protasi.
Pia alizitajata timu ambazo hazikushiriki katika ligi daraja la kwanza kwa mssimu wa 2010/2011 kuwa ni Polisi Mara, Polisi Kigoma, Magereza Tabora Maganga ya jiji la Dar es Salaam pamoja na F11 Quens ya Gongo la Mboto katika jiji la Dar es Salaam.
Pia alitaja timu ambazo hazikuweza kucheza hatua ya robo fainali kuwa ni timu mwenyeji ya Mzinga Morogoro, Black Sisters kutoka mkoani Pwani na Tupendane ya mkoa wa Lindi.
0 comments:
Post a Comment